February 22, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Rais Samia aikumbuka barabara ya Katerero-Ibwera-Izimbya-Katoro hadi Kyaka

Rais Samia Suluhu Hassan

 

MKURUGENZI wa Mipango ya Miundombinu wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Ephatar Mlavi,amesema kuwa katika kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa Madaraja makubwa dara la Karebe katika Mkoa wa Kagera ni mojawapo kutokana na umuhimu wake. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Akizungumza na vyombo vya habari katika ukumbi wa habari Maelezo Mhandisi Mlavi amesema kuwa kwa sasa serikali imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kutekeleza miundombinu ya barabara iliwa ni pamoja na ujenzi wa madaraja makubwa 9 nchini.

“Jumla ya madaraja makubwa 9 yamekamilika kujengwa kwa gharama ya Sh. 381.3 bilioni na madaraja mengine kumi ujenzi wake unaendelea kwa gharama ya shilingi Bilioni 985.802. Jumla ya madaraja makubwa 19 yapo kwenye maandalizi ya kujengwa,” ameeleza Mhandisi Mlavi.

Akizungumzia barabara ya siku nyingi na yenye umuhimu wa usafirishaji bidhaa mabalimbali ya kutoka Katerero, Ibwera, izimbya Katoro hadi Kyaka ambayo ipo jimbo la Bukoba Vijijini Mhandisi Mlavi amesema kuwa barabara hiyo ni muhimu na ipo katika bajeti ya kujengwa kwa kiwango cha lami.

Mkurugenzi wa Mipango ya Miundombinu (TANROAD), Mhandisi Ephatar Mlavi

Amesema katika kutambua umuhimu wa barabara hiyo tayari wameanza nanujenzi wa daraja la Karebe na kuhakikisha barabara hiyo inatumika kwa urahisi kwa kipindi chote cha mwaka.

Barabara hiyo ni kati ya barabara muhimu zilizopo katika jimbo la Bukoba vijijini na barabara hiyo haijawahi kutengenezwa kwa kiwango cha lami lakini kwa uongozi wa serikali ya awamu ya sita ipo kwenye mpango wa matengenezo kwa kiwango cha lami.

Mhandisi Mlavi amesema kuwa kwa sasa Barabara zenye urefu wa jumla ya kilometa 15,625.55 zimekuwa katika hatua mabalimbali za utekelezaji ambapo barabara zenye urefu wa jumla ya kilometa 1,365.87 zimekamilika kujengwa kwa kiwango cha lami.

Ameeleza kuwa barabara zenye urefu wa jumla ya kilometa 2,031.11 zimeendelea kujengwa kwa kiwango cha lami huku upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara zenye jumla ya kilometa 4,734.43 na madaraja kumi unaendelea.

About The Author

error: Content is protected !!