February 12, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Rais Mwinyi amuapisha Kamshna mpya wa ZRA

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amemuapisha Said Kiondo Athumani aliyemteuwa hivi karibuni kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka Mapato (ZRA). Anaripoti Apaikunda Mosha. Zanzibar …(endelea).

Rais Dk. Mwinyi mnamo Februari 8, 2025, alifanya uteuzi huu, kufuatia aliyekuwa Kamishna Mkuu wa ZRA, Yussuph Juma kumaliza muda wake na leo ameungana na baadhi ya viongozi mbalimbali Ikulu Zanzibar ili kufanya hafla hiyo ya uapisho.

Kamishna Kiondo amemshukuru Rais Dk. Mwinyi na serikali yake kwa kumwamini na kwa kumteua katika nafasi hiyo muhimu. ameahidi kuendelea kuimarisha uhiari wa kulipa  kodi kwa kuwashirikisha walipa kodi kwa kuwahamasisha, kuwapa elimu na ushawishi kulipa kodi kwani ni kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

“Zama za kulazimisha ulipaji kodi zimepitwa na wakati, na sasa ni muhimu kushirikiana kwa maelewano na kueleza umuhimu wa kodi kwa maendeleo ya taifa,” alisema.

Kabla ya Uteuzi huo Kamishna Kiondo alikuwa Mkufunzi Mkuu wa Chuo cha Kodi cha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

Aidha, Kaimu Kamishna Mkuu wa ZRA, Said Ali Mohammed, alimkabidhi rasmi ofisi Kamishna Kiondo na kumhakikishia ushirikiano wa dhati katika kuhakikisha malengo ya mamlaka hiyo yanafanikiwa kwa ufanisi zaidi.

About The Author

error: Content is protected !!