
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei ya ukomo ya mafuta kuanzia leo, tarehe 5 Februari 2025, kwa rejareja katika jiji la Dar es Salaam zimeongezeka kama ifuatavyo:
• Petroli imepanda kwa asilimia 0.96% kutoka Sh2,793 hadi Sh2,820 kwa lita.
• Dizeli imeongezeka kwa asilimia 2.18%, kutoka Sh2,644 hadi Sh2,703 kwa lita.
• Mafuta ya taa yameongezeka kwa asilimia 1.25%, kutoka Sh2,676 hadi Sh2,710 kwa lita.
Ongezeko hili linatarajiwa kuathiri gharama za usafiri na shughuli nyingine zinazotegemea nishati hii.
ZINAZOFANANA
Serikali yajivunia mafanikio sita ya TASAF
Dk. Kimei aweka rekodi ya utendaji Vunjo
Bashe atoa onyo kwa wasafirishaji wa bidhaa za kilimo Malawi na Afrika Kusini