January 30, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

‘Honey Moon’ yenu ikija na mambo ya hovyo hatukubali – Wassira

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira Chama na serikali yake haitakubaliana na azimio lolote litakalopitishwa na Chama cha Demokrasia na maenddeleo lenye lengo la kuvunja amani, umoja na mshikamano wa taifa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mara … (endelea).

Amesema amesikia chama hicho kikitangaza kwamba kinakwenda kujifungia halafu kije na jambo ambalo halijapata kushuhudiwa nchini, hivyo anatoa angalizo mapema kuwa jambo hilo ni lazima lifuate katiba, sharia, kanuni na miongozo ya nchi endapo halitazingatia hayo CCM haitakubaliana nao.

Wasira alisema hayo jana mjini Bunda alipohutubia wananchi katika mkutano uliotumika kuzindua sherehe za maadhimisho ya miaka 48 ya kuzaliwa kwa Chama kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Stendi ya zamani.

“Wamesema wanajifungia halafu waje wafanye jambo ambalo halijapata kuonekana, nikasema ni jambo gani, mimi nikaona huko kujifungia ile ni honeymoon maana honeymoon simnaijua, watu wakishaoana wanajifungia mahali…ile ni honemoon.

“Tunawaambia tunawatakia heri kwenye honeymoon lakini tunawaambia lolote watakalotoka nalo kwenye honeymoon lazima lifuate sheria, waklija na honeymoon inavunja amani hatuwezi kuwaunga mkono.

“Amani sera ya msingi ya Chama chetu na nchi yetu, sisi ni tofauti na nchi nyingine za Afrika hatujapigana wenyewe kwa wenyewe wala hatujapata kupinduana kwa hiyo hatuwezi kuruhusu kikundi cha watu kivuruge amani na tunawaambia katika suala la amani hakuna msalie mtume, tutalinda amani ya Tanzania kswa gharama yoyote,” alisema.

Alisema Tundu Lissu ameona ukweli na umuhimu wa uchaguzi ndio maana ameamua hawezi kugomea uchaguzi “namkaribisha sana katika uwanja wa mapambano maana hilo ndilo jambo la msingi kwamba tutagombea naye.”

Wasira alisema ana hakika CCM itapata ushindi wa kishindo katika juchaguzi mkuu wa mwaka huu kutokana na mambo makubwa yaliyofanyika katika utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi.

“Ataweka wagombea, ila tunachomwambia ni kwamba tumejipanga kushinda kwa kishindo, tutashindana naye kwa udiwani, tutashandana nao kwa ubunge lakini kwa urais ikulu wataiona kwa luninga.

“Utaenda kupiga kura kwa chama kingine ili upate nini, maana hupigi kura kwa furaha tu, unapiga kura kwa jambo linalokuhusu.

“Rais wetu ni mwenye upendo mkubwa ameanzisha sera inaitwa 4R moja ni maridhiano na sisi CCM ni Chama kinachopigania amani, sisi ni Chama kinachosimamia maendeleo, sisi ni Chama kinachopigania umoja wa watu wa Afrika, hizo ndizo sera zetu za msingi.

Alisema kuwa CHADEMA imeshindwa kutumia fursa iliyotolewsa na Rais Samia ya kukaa pamoja na kujadili mambo ya msingi yanayohusu mustkabali wa taifa.

“Rafiki zetu wale walikuja wakasema hali ni mbaya sana turidhiane, wakaleta ajenda wanasema tuwaruhusu waliokimbia warudi na kwamba watakuwa salama, walirudi na wako salama, wakasema wana watu 400 ambao walikamatwa walifunguliwa kesi na wengine walifungwa wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 wakasema waachiliwe lakini kuachiliwa kama una kesi kuna utaratibu wake, utaratibu ukafuatwa wakaachiwa na waliokuwa wamefungwa wakasamehewa kwa msamaha wa rais chini ya mamlaka yake kwa mujibu wa katiba. Hilo wakapata.

Wakasema tunataka mikutano na maandamano, wakapewa mikutano na maandano hata Bunda walikuja na helkopta yao na ninyi watu wa Bunda mkawasikiliza lakini hamna kitu, nilikuwa nawasikiliza watasema nini, wakawa wanasema katiba katiba, sasa hawa wananchi wanataka chakula, wanataka hospitali wewe kila siku ukija unasema katiba katiba, hawana hoja.

“Wakasema tufukuze wale kinamama 19 (wabunge wa viti maalumu kutoka CHADEMA) waliokuwa bungeni tukasema wana kesi hatuwezi kwenda kuiamuru mahakama hatuna mamlaka hayo. Wakasema tumekataa.

“Wakasema tufanye siri na CHADEMA tuunde katiba tukasema katiba haiundwi na vyama vya siasa inaandikwa na wananchi na hatuwezi kula njama dhidi ya Watanzania, sisi ni Chama cha watu wote hatuwezi kula njama dhidi yao,

“Walipoona tumekataa mambo yao yasiyo na msingi wakajitoa katika mazungumzo wakasema sasa maridhiano hakuna, sisi tukasema maridhiano ni sera haihusu CHADEMA peke yake tunaridhiana na kila mtu sasa hapo ndipo tulipo,” alisema Wasira akikumbusha hatua mbalimbali zilizofanywa na CCM kuleta maridhiano.

Wasira alisema hatua mbalimbali zimechukuliwa kutokana na maombi na mapendekezo ya wadau ikiwemo kubadilisha sharia za uchaguzi ikiwemo kuwa na tume huru ya uchaguzi hoja ambayo imetekelezwa.

About The Author

error: Content is protected !!