MWENYEKITI Mstaafu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema pamoja na kuwa yeye ni mstaafu lakini anatoa maagizo ya viongozi wapya wa chama hicho kuunda tume kwa ajili kuyaponya majeraha yaliyotokana na kampeni za uchaguzi uliomuondoa madarakani. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).
Mbowe ameyasema hayo leo tarehe 22 Januari 2025 alipokuwa akiwaaga wajumbe na wanachama wa chama hicho.
“Kwa namna wagombea mbalimbali walifanya kampeni zao zimeacha majeraha mengi tusipolitibu jambo hili litaharibu brand ya chama chetu,” alisema Mbowe na kuongeza.
“Mimi niliahidi nikishinda nitaunda tume ya kuponya majeraha yaliyotokana na uchaguzi nazungumza kama Baba wa Chama hichi nawaagiza katibu majeraha haya undeni tume haraka ya kuponya majeraha.”
Mbowe amesema kuwa anawaagiza viongozi walioingia madarakani wasifanya jambo kinyume cha Katiba ya chama hicho.
ZINAZOFANANA
Lissu amzidi Mbowe kura 31, Heche Makamu Mwenyekiti Bara
Lissu: Sijawahi kugombana na Mbowe
Mbowe afungua Mkutano Mkuu akilia na matusi