MWANAHARAKATI wa haki za Binadamu Maria Sarungi, raia wa Tanzania amepatikana mara baada ya kutekwa na watu wenye silaha nchini Kenya, leo mchana. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Taarifa za kutekwa kwa mwanaharakati huyo, zilitolewa leo mchana tarehe 12 Januari 2025, kupitia shirika la kimataifa la Amnestry International kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii.
Taarifa ya shirika hilo lilisema kuwa, Maria alitekwa na wanaume watatu waliokuwa na Silaha na ambao walikuwa na gari nyeusi aina ya Noah, katika eneo la Chaka Place, mtaa wa Kilimani mjini Nairobi.
Taarifa za kupatikana kwa Maria zilikuja Saa chache zilizopita, mara baada ya kuposti video kupitia kuraza yake ya mtandao wa kijamii wa ‘X’ zamani Twitter, akishukuru kila mmoja ambaye alipaza sauti.
“Mungu ni mwema Nimepambana na ninyi mmepambana, kwa sasa nipo salama, shukrani kwa kila mmoja, nitaongea zaidi kesho nawapenda sana!” Aliandika Maria
ZINAZOFANANA
NIDA kutoa vitambulisho laki 4, waboresha mfumo
Maria Sarungi atekwa nchini Kenya
Serikali yasisitiza umuhimu wa mafunzo ya ufuatiliaji miradi yake