January 8, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Makala apata kigugumizi kinachoendelea Chadema

Amos Makala, Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM

 

LEO Januari 7 2025 Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Amos Makala amekataa kuzungumzia mihemuko ya baadhi ya makada wa chama hicho kuhusu uchaguzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Makala amegoma kuzungumzia masuala hayo baada ya waandishi kutaka kujua mwenendo wa makada wa chama hicho kutokana na tabia ya baadhi yao kumpigia chapuo, Tundu Lissu aliyetangaza kugombea nafasi ya uenyekiti kupitia chama cha Chadema.

Wakati huo huo, Makala amevunja ukimya wa muda wa takribani zaidi miezi sita tangu amejiuzuru nafasi ya umakamu mwenyekiti Abdulrahman Kinana kwa kuachia ngazi Julai 2024.

Kutokana na kuachia ngazi Kinana na muda mrefu mijadala ilianzishwa na kutaka kujua nani anachukua nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa (CCM).

Ili kuzima mijadala hiyo hatimaye leo Januari 7,2025 Makala ametoa ufafanuzi na kueleza kuwa mrithi wa Kinana anatarajiwa kupatikana kati ya January 18 au 19 mwaka huu.

Akizungumza leo Januari 7,2025 Jijini Dodoma, Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama hicho, Amos Makala ameeleza kuwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti huwa haigombewi wala kujazwa fomu bali hutokana na mapendekezo ya Mkutano Mkuu na halmashauri kuu ya CCM.

Amesema kuwa hatua hiyo ni mara baada ya aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, Abdulrahman Kinana kutangaza kustaafu kwenye nafasi hiyo tangu Julai mwaka jana kwa madai ya kutaka kupumzika ambapo Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuridhia ombi lake.

“Niwaombe wanachama watu kuachana na taharuki zinazoendelea kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mrithi wa Makumu Mwenyekiti wa chama Abdulahman Kinana, nafasi hii haigombewi ila inapendekezwa,” ameeleza Makala.

Makala amewaambia waandishi wa habari kuwa kwa sasa hakuna mchakato wowote wa mrithi wa nafasi hiyo ambaye atapatikana baada ya mapendekezo ya jina katika kikao cha Kamati kuu na Halmashauri kuu Taifa.

” Wale waliokuwa wakibashiri mrithi wa Kinana muda huo haupo badala yake mrithi tutampata kwa jina kupendekezwa kwenye vikao na tayari maandailizi yote yanaendelea kufanyika kupitia Katibu mkuu wa Chama chetu Emmanuel Nchimbi, hivyo tuache taharuki CCM kinaendeshwa kwa Katiba na utaratibu,”amesema

Wakati huo huo Katibu Mwenezi huyo ametoa taarifa juu ya uwepo wa Mkutano Mkuu CCM January 18 hadi 19 2025 ambapo ameeleza kuwa Mkutano huo utaendana na vikao vya Kamati kuu na Halmashauri kuu Taifa.

About The Author

error: Content is protected !!