CHAMA cha Mapinduzi (CCM), kimepongeza mchango mkubwa unaotolewa na Mkurugenzi wa shule za Tusiime za Tabata Sanene jijini Dar es Salaam, Dk. Albert Katagira kwa chama hicho mara kwa mara. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Pongezi hizo zilitolewa mwishoni mwa wiki na Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa Wazazi, Sudi Kassim Sudi, kwenye kikao chao kilichofanyika mwishoni mwa wiki kwenye ukumbi wa shule hizo jijini Dar es Salaam.
Sudi alisema Mkurugenzi wa shule hiyo Dk. Katagira ameonyesha upendo wa hali ya juu na kukiheshimisha chama hicho kutokana na michango yake ya mara kwa mara.
“Mapokezi tuliyopata hapa Tusiime na heshima tuliyopewa tunaahidi kurudi tena kufanya mkutano wetu hapa mwakani, nakushukuru sana tulikuwa na kijana wako na watumishi wengine walitupa ushirikiano wote, kila mara walikuwa wakituuliza tunataka nini,” alisema.
“Mwanangu kasomashule hii kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne na kwa bahati nzuri kapata daraja la kwanza, hii shule inamaadili ya kiislamu na kikristu, nyie ni mashahidi mmekuja hapa mkiwa na imani ya kiislamu lakini mmesali bila tatizo na wakristo nao wamewekewa mazingira mazuri ya kufanya ibada,” alisema.
“Mimi kwa nafasi yangu kama Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa ntaendelea kukutangaza hadi kwenye mikutano ya Baraza Kuu Dodoma kwasababu wewe unatoa fursa kwa chama hicho,” alisema.
ZINAZOFANANA
Ushindi wa Profesa Lipumba wapingwa
Sativa amlipia Lissu fomu ya kugombea Uenyekiti Chadema
John Tendwa afariki dunia