RABAT. Morocco inalenga kuwapa wanawake haki zaidi ya malezi pamoja na kupinga ndoa za wake wengi, katika mapitio ya kwanza ya kanuni za familia katika kipindi cha miaka 20, mawaziri wa haki na masuala ya Kiislamu walisema Jumanne. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, wanaharakati wa kutetea haki za wanawake wamekuwa wakishinikiza kupitiwa tena kanuni zinazosimamia haki za wanawake na watoto ndani ya familia nchini Morocco, ambako Uislamu ni dini ya serikali.
Rasimu ya kanuni inapendekeza zaidi ya marekebisho 100, hasa kuruhusu wanawake kupinga ndoa za wake wengi, waziri wa sheria Abdellatif Ouahbi aliwaambia waandishi wa habari.
Pia inalenga kurahisisha taratibu za talaka, inazingatia ulezi wa mtoto kuwa ni haki ya pamoja kati ya wanandoa na inampa kila mwanandoa haki ya kuhifadhi nyumba ya ndoa endapo mwenzake atafariki, alisema.
Wanawake walioachwa wataruhusiwa kuendelea kutunza mtoto baada ya kuolewa tena.
ZINAZOFANANA
Jeshi la Polisi: Sherekeheni sikukuu kwa utulivu na amani
Ushindi wa Profesa Lipumba wapingwa
Ukraine wakiri kufanya mauaji ya Jenerali wa Urusi na msaidizi wake mjini Moscow