MBUNGE wa zamani wa Bukoba mjini, Wilfred Lwakatare ambaye ni mgombea nafasi ya uenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), amesema kuwa endapo Profesa Ibrahimu Lipumba atadhihirisha nia ya kugombea uenyekiti wa chama hicho atajiondoa kuwania nafasi hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Akizungumza na MwanaHALISI Online leo tarehe 16 Desemba 2024, Lwakatare amesema kuwa atachukua hatua hiyo kwa kuwa anamheshimu Profesa Lipumba na kwamba kitendo kushindana naye hakina afya kwake.
“Mimi ndiye mtu wa kwanza kumshawishi Profesa Lipumba kwa mara ya kwanza kuwania nafasi ta uenyekiti, leo kama atasema anagombea nitajitoa” amesema Lwakatere.
Uchaguzi Mkuu wa CUF unatarajiwa kufanyika tarehe 18, 19 Desemba 2024 .
Mpaka sasa Profesa Lipumba hajatoka hadharani kuthibitisha kuwa atakugombea ingawa baadhi ya wanachama wameshamchukulia fomu.
Ukimya wa Profesa Lipumba umewagawa wanachama ambapo baadhi wanataka astaafu kwa heshima huku wengine wanataka aendelee.
Wagombea wengine ni Maftaha Nachuma Makamu Mwenyekiti-Bara, Jafari Mneke, Hamad Masoud Katibu Mkuu wa chama hicho.
Prof. Lipumba amekalia kiti hicho kuanzia mwaka 1995 mpaka leo hivyo kumfanya kuwa mwenyekiti wa muda mrefu zaidi kwenye vyama vya siasa nchini kwa kudumu kwa takribani miaka 30.
ZINAZOFANANA
Januari 21, 2025 kusuka ama kunyoa Chadema
Prof. Kitila: Lissu ameudanganya Umma, hatukupanga mapinduzi
Lissu ataka Chadema mpya kwenye uongozi wake