JUMLA ya wanafunzi wa kike 2,600 wamejengewa uwezo wa masomo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na Kampuni ya simu ya Mikononi ya Vodacom Tanzania tangu 2018 mpaka mwaka huu kupitia program ya Code Like a Girl. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Mkuu wa Kanda ya kati wa Vodacom Tanzani, Joseph Sayi alisema hayo leo desemba 13 wakati alipokuwa akifunga mafunzo hayo ya TEHAMA yaliyofanyika Chuo kikuu cha Dodoma (Udom).
Alibainisha kuwa mafunzo hayo yamekuwa yakitolewa kwa awamu kwa baadhi ya Mikoa hapa nchini yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo wa masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati (STEM) wanafunzi hao wa kike kwa ufadhili wa Vodacom Tanzania PLC.
Meneja wa Kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania Kanda ya Kati ,Joseph Sayi (kulia) akizungumza na wanafunzi wasichana kutoka Kanda hiyo wakati wa kufunga mafunzo ya kuwajengea uwezo katika masomo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) yaliyofanyika Chuo Kikuu cha Udom Jijini Dodoma jana kwa ufadhili wa Vodacom.
Meneja wa Kampuni ya Vodacom Tanzania Kanda ya Kati Joseph Sayi (kushoto) akimkabdhi cheti mwanafunzi Winnie Futa wakati wa kufunga mafunzo ya kuwajengea uwezo wanafunzi wa kike katika masomo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) yaliyofadhiliwa na Vodacom.
Meneja wa Kampuni ya Vodacom Tanzania Kanda ya Kati Joseph Sayi (kushoto) akimkabidhi begi mwanafunzi Emmeline Kitali wakati wa kufunga mafunzo ya kuwajengea wanafunzi wa kike uwezo wanafunzi wa kike katika masomo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) yaliyofanyika Chuo kikuu cha Udom Jijini Dodoma jana kwa ufadhiliwa na Vodacom.
Baadhi ya wanafunzi wa kike kutoka shule za sekondari Kanda ya kati wakijifunza jinsi ya kutumia kopyuta kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo katika masomo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA ) yaliyofanyika Chuo kikuu cha Udom Jijini Dodoma jana kwa ufadhili wa kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom Tanzania.
ZINAZOFANANA
Waziri Jafo akagua maandalizi miaka 60 ya CBE
Siku mbili zimebaki milioni moja itoke kupitia shindano la Expanse
Shindano la Expanse Kasino ndio habari ya mjini kwa sasa