December 12, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Wanandoa waiomba Mahakama Kuu ipitie mwenendo wa kesi yao Kisutu

 

WANANDOA Bharat Nathwan (57) na Sangita Bharat (54) wanaotuhumiwa kwa kesi ya kujeruhi na kutoa lugha ya matusi wameandika barua Mahakama Kuu kwa Jaji Mfawidhi wakiomba Mahakama ipitie mwendenendo wa kesi yao hiyo iliyopo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea). 

Aidha, wameomba Mahakama ya Kisutu itumie busara kusimama kusikiliza kesi hiyo hadi pale barua yao itakapojibiwa kwa sababu tayari imeshamfikia Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, kwa hali hiyo suala hilo linafanyiwa kazi.

Ombi hilo limetolewa leo Desemba 10, 2024 washtakiwa hao kupitia Wakili wao Edward Chuwa na Anna Lugendo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Aaron Lyamuya wa mahakama ya Kisutu wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.

Amedai kuwa wapo tayari kuendelea na kesi lakini wanahoja wanataka iingie kwenye rekodi za Mahakama kwamba Wakili mwenzake Gabriel Mnyele amemuandikia barua jaji huyo ili aweze kuangalia mwenendo wa kesi hiyo ili aweze kutoa uamuzi.

“Kama Mahakama itaona busara iendelee na usikilizwaji wa kesi hii na wakati maombi yapo Mahakama Kuu basi iendelee,”ameai Wakili Chuwa

Hata hivyo, Wakili wa Serikali Faraji Ngukah alidai kuwa hawana pingamizi kwa sababu ni haki yao kuomba, lakini haizuii chochote kesi kuendelea hivyo wanaomba kesi hiyo iendelee kusikilizwa na zuio litakapotolewa kesi itasimama kusikilizwa.

Wakili Chuwa alidai kuwa tayari wateja na mawakili wanataka mwenendo uangaliwe upya, kwa hiyo nakusihi usisikilize kwa sababu Mahakama Kuu imeshaanza kulifanyia kazi, tayari lipo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu

“Nakusihi sana utumie busara kwa muda mchache tu ili niweze kufuatilia kwa Jaji Mfawidhi Mahakama, haki ya kulalamika ni ya kila mtu, kwa hiyo tuache kwanza nifuatilie,”ameomba wakili Chuwa.

Hakimu Lyamuya baada ya kusikiliza hoja zao, amesema kesi hiyo imekuwa na mambo mengi sana ndiyo maana ameamua kuihamishia chumba cha wazi cha Mahakama kwa ajili ya watazamaji (Audience) wao ndiyo watakao hukumu nasikiliza kesi vizuri au vibaya.

“Mmeeleza kwamba mmeandika barua kwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, utaratibu ni kwamba unapotaka kufanya jambo huko unafanya maombi rasmi na sio barua, inaweza ikasomwa na isifanye chochote,”alisema Hakimu Lyamuya

Amesema barua haiwezi kuihamisha mahakama, Jaji akitaka mwenendo wa kesi anaangalia moja kwa moja kwa kila kitu kipo kwenye mtandao kwa kila kitu ana kiona.

“Hadi hivi sasa sioni chochote hapa, mnachosubiri nyinyi ni kudra zake tu, hamjui ni lini hiyo barua kujibwa. Nisingeahirisha kesi kwa sababu hii mwenendo wa kesi ungekuwa ni batili, Mnyele hayupo mara ya pili nampa nafasi nyingine,”amesema

Hakimu Lyamuya ameema anaahirisha kesi hiyo kwa sababu Mnyele hayupo na washtakiwa wana haki ya kuwa na uwakilishi na pia katika utendaji kazi wake hajawahi kuona barua imeandikwa kesi ikaahirishwa.

Hata hivyo, Wakili Ngukah alidai hana pingamizi na uamuzi wa kiti, lakini walitaka kujua Chuwa awaeleze Mnyele yuko wapi, Hakimu Lyamuya aliwaeleza kwamba kila mtu na haki ya kupewa nafasi nyingine, kwa hiyo amitoa kwa wakili huyo.

“Natoa maelekezo kwa washtakiwa naomba mnisikilize kwa makini nyie ndiyo imeweka mawakili Januari 7,2025 kama wakili wenu hata kuja tutaendelea bila yeye kuwepo zingatieni sana nyie ndiyo washtakiwa hakuna wengine ni nyie,”alisema

Wanandoa hao ambao ni raia wa Tanzania asili ya kihindi wanaoishi Mtaa wa Mrima – Kisutu, jengo la Lohana Dar es Salaam wanaotuhumiwa kwa mashtaka manne waliyoyatenda Julai 21,2023 kinyume cha sheria.

Ilidaiwa kuwa Nathwan anatuhumiwa Julai 21,2023 akiwa eneo la mtaa wa Mrima-Kisutu, jingo la Lohana, ndani ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam kinyume cha sheria alimsababishia madhara makubwa Kiran Lalit kwa kuzamisha kichwa chake kwenye ndoo la saruji iliyochanganywa.

About The Author

error: Content is protected !!