MAMLAKA ya Usimamizi waBandari Tanzania (TPA) kwa mara ya tatu mfululizo imetangazwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kuwa ni mwajiri bora wa sekta ya umma na kupea Tuzo ya Mwanachama wa Kudumu kwa Taasisi za Umma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Da es Salaam … (endelea).
Akikabidhi uongozi wa TPA tuzo za umahili mwishoni mwa juma hapa, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko, amewapongeza wafanyakazi na viongozi wa TPA kwa ushindi wa tuzo hizo na kuitaka mamlaka kuendeleza juhudi ambazoo zimeifanya ishinde tuzo mara tatu mfululizo.
Dk Biteko amekumbusha kwamba TPA ni taasisi ya kitaifa ya kiuchumi na kimkakati na kueleza furaha yake kwa utendaji wa TPA ambao umetambuliwa na ATE pasipo upendeleo wowote. Alisema TPA siyo tu inafanya vizuri kiuchumi bali imeonyesha kwamba ni mwajiri wa kupigiwa mfano nchini.
Dk Biteko alimwakilisha Makamu wa Rais, Dr Philip Mpango katika hafla hiyo na kuwafikishia wafanyakazi na uongozi wa TPA salamu za Makamu wa Rais za kuwatakia mafunikio katika siku zijazo.
Naibu Waziri Mkuu aliwaelezwa kwamba TPA haikushinda tu Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka katika sekta ya umma, bali pia imetwaa tuzo nyingine nne ikiwemo Tuzo ya Mwajiri Bora Mzawa (Local Employer Award), mamlaka ikiwa mshindi wa kwanza; TPA pia ilitangazwa kuwa mshindi wa pili wa jumla kwa sekta zote na kupewa Tuzo ya 2nd Runners-Up.
Aidha TPA ilitambuliwa kama moja ya taasisi zinazofanya vizuri sana na kupewa Tuzo ya Club of Best Performers na kupongezwa kwa uanachama wa muda mrefu wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) na kupewa Tuzo ya Mwanachama wa Kudumu kwa Taasisi za Umma.
Dr Biteko alifahamishwa kuwa tuzo hizi hutolewa kila mwaka na ATE kwa waajiri kutoka sekta za umma na binafsi ambao wameonyesha utendaji bora na ubunifu katika mwaka husika. Ilielezwa kuwa ushindi wa TPA ni uthibitisho wa dhamira yake ya kuboresha ustawi wa wafanyakazi, kuboresha mazingira ya kazi na kuendelea kuchangia maendeleo ya sekta ya bandari nchini.
Mwaka huu TPA ilitowa kwa serikali gawio la shilingi bilioni 153.9 na kuwa taasisi iliyotoa gawio la juu kabisa. Kampuni 145 zilikabidhi kwa Rais Samia Suluhu Hassan jumla ya shilingi bilioni 636 ikiwa ni gawio kwa serikali. Taasisi za kibiashara zilitoa 278bn/- na mamlaka za udhibiti zilitoa 358bn/-.
ZINAZOFANANA
Chuo Kikuu cha Marekani kutunuku shahada ya Udaktari kwa watanzania wanne
Serikali yatia nguvu ubunifu na utafiti kuzikabili changamoto za uchumi na jamii
Wamilikiwa Jengo la Kariakoo wapandishwa kizimbani kwa mauaji bila kukusudia