January 2, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Wamilikiwa Jengo la Kariakoo wapandishwa kizimbani kwa mauaji bila kukusudia

 

WATU watatu ambao ni wamiliki wa jengo la Ghorofa la Kariakoo lilioporomoka Novemba 16 Mwaka huu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashataka 31 likimewo mauaji bila kukusudia. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Leo tarehe 29 Novemba 2024 wakili wa serikali Adolf Lema, Grace Mwanga na Erick Kamala Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Godfrey Mhina wamewasomea mashatka 31 watuhumiwa hao.

Watuhumiwa hapo ni pamoja na Ashour Awadh Ashour (38), Mkazi wa llala, Leondela Mdete (49), Mkazi wa Mbezi Beach na Zainab Islam (61), Mkazi wa Kariakoo .

Kwa pamoja watatu hao wanadaiwa kuwa ni Wamiliki wa jengo lililoanguka Mtaa wa Mchikichi na Congo, Kariakoo jijini Dar es Salaam na kusabanisha vifo vya Watu 29.

Inadaiwa siku ya tukio isivyo halali, washtakiwa walishindwa kutimiza majukumu yao na kusabashisha vifo vya Said Juma, Hussein Njou, Prosper Mwasanjobe, Shadrack Mshingo, Godfrey Sanga, Neema Sanga, Elizabeth Mbaruku, Hilary Minja, Abdul Sululu, Chatherine Mbilinyi na wengine 21

Hata hivyo washtakiwa wamekana kutenda kosa hilo na mshtakiwa Mdete ameachiwa huru kwa dhamana wakati mshtakiwa Islam na Ashour wakirudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambayo yaliwataka kuwa na
wadhamini wawili kila mmoja wenye barua za utambulisho, kitambulisho cha Taifa na walitakiwa kusaini bondi ya Shilingi Milioni Tano kwa kila mmoja

About The Author

error: Content is protected !!