WAKATI joto la Uchaguzi likipanda Jeshi la Polisi mkoani Singida linamshikilia askari wa Jeshi la Magereza kwa tuhuma za mauaji ya George Mohamedi mgombea uenyekiti kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wa kitongoji cha Stand Manyoni mkoani humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Singida … (endelea).
Awali Taarifa ya John Mrema, Mkurugenzi Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya nje wa Chadema iliyotolewa leo tarehe 27 Novemba 2024 ilisema kuwa Mohamedi aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa nyumbani kwake baada ya kuvamiwa na makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Taarifa ya jeshi la Polisi mkaoni humo inaeleza kuwa linamshikiria askari wa Magereza kwa kusababisha kifo cha mgombea huyo jana tarehe 26 Novemba 2024, saa tano usiku.
Taarifa ya Polisi inasema kuwa wafuasi wa CCM walikuwa wana kikao cha ndani katika moja ya nyumba za eneo hilo nawakati kikao hicho kinaendeleo walivamiwa na kundi la wafuasi wa Chadema.
“…Askari Magereza ambao wapo katika gereza lilikuwepo karibu na eneo hilo walitaarifiwana wakafika haraka , wakati askari hao wanakwenda waliwasiliana na polisi walipofika eneo la tukio walishambuliwa kwa mawe hali ambayo iliwalazimisha kupiga risasi hewani kutuliza purukushani risasi hizo moja ilimjeruhi Mohamedi”
ZINAZOFANANA
Dk. Faustine Ndungulile afariki dunia
Ushiriki wa Rais Samia G20 wainufaisha Tanzania
Polisi wadai Chadema wamewapiga mawe