SERIKALI imekipa Chuo cha Kodi (ITA), jukumu la kufanya utafiti wa namna ya kuongeza idadi ya walipa kodi, kubaini vyanzo vipya pamoja na ukusanyaji wa kodi katika biashara za mitandaoni na zile za kimaifa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Hayo yamesemwa leo katika mahafali ya 17 ya chuo hicho yaliyofanyika leo tarehe 22 Novemba 2024.
Hayo yalisemwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Elijah Mwandumbya wakati akimwakilisha Waziri wa Fedha dk Mwigulu Nchemba kwenye Mahafali ya kumi na saba ya Chuo cha Kodi (ITA) ,Dar es salaam jana.
“Chuo kijikite na tafiti zitakazotoa changamoto kwenye mfumo wa ukusanyaji wa kodi na forodha kwani mapendekezo mengi yanayotolewa na jamii yanakosa utafiti au vithibitisho hivyo kufanya mwendelezo wa mapendekezo kuongezeka kwani hatujakidhi na kufikia malengo wanayoyataka,”alisema Mwandumbya.
Aidha Mwandumbya alisisitiza Chuo kiendelea kutoa mafunzo ya viwango vya juu huku kikizingatia kasi ya maendeleo ya sayansi na teknolojia kwani ndipo dunia inapoelekea kwa sasa hasa katika matumizi ya akili mnemba.
Mwandumbya aliwataka wahitimu kushiriki katika kukuza pato la Taifa kwa kukusanya kile kinachostahili na watu kulipa kile wanachotakiwa kulipa hasa katika biashara za mitandaoni ama kimataifa ili serikali ikamilishe miradi yake.
Kwa upande wake Kamishna Mkuu wa Kodi Tanzania (TRA), Yusuph Mwenda alisema baraza lililopo liendelee kufanya kazi kwa uweledi ili kufanikisha watumishi kupata elimu itakayowezesha kuongeza idadi ya walipa kodi kwa hiari na kuboresha miundombinu bora kwa maendeleo ya nchi.
Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Isaya Jairo alisema Chuo kimetengeneza wataalamu wengi wa forodha na kodi kwenye misingi ya kujenga umahiri na kukuza uchumi wa Taifa pamoja na kutumia fursa za uendeshaji wa teknolojia na sayansi na itasaidia wahitimu hao waendane na kasi ya teknolojia na forodha ya dunia ya sasa.
Chuo hicho kimetunuku vyeti kwa wahitimu 417 wa kozi mbalimbali kwa mwaka wa masomo 2023/2024 huku idadi hiyo wanaume ni 236 na wanawake 181 ambapo195 wametunukiwa cheti cha Uwakala wa forodha wa Afrika Mashariki(EACFF), Wahitimu 28 wametunukiwa Cheti cha Usimamizi wa Forodha na Kodi (CCTM), 61 wametunukiwa Stashahada ya Usimamizi wa Forodha na kodi (DCTM), 119 wametunukiwa Shahada ya Usimamizi wa Forodha na Kodi (BCTM) na Wahitimu 14 wametunukiwa Stashahada ya Uzamili katika Kodi (PGDT).
ZINAZOFANANA
Benki ya NBC yatambulisha kampeni ya Kilimo Mahususi kwa wakulima na wafugaji Mbeya
Upelelezi wakwamisha kesi ya Boni Yai
Wahitimu 417 kutunikiwa vyetu ITA