November 23, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Polisi wadai Chadema wamewapiga mawe

 

JESHI la Polisi mkoani Songwe, limethibitisha kuwashilikia viongozi kadha wandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), akiwamo mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe. Anaripoti Mwandishi Wetu, Songwe  … (endelea).

Taarifa ya jesho hilo, iliyotolewa leo 22 Septemba 2024, imewataja waliokamatwa pamoja na Mbowe, kuwa ni Joseph Mbilinyi, mwenyekiti wa chama hicho, Kanda ya Nyasa; Pascal Haonga, mbunge mstaafu wa Mbozi – Mlowo, Mdude Nyagali na Apolinary Margwe, Afisa wa Habari wa chama hicho.

Wengine, ni Adam Kasekwa (Adamoo), mlinzi wa mwenyekiti wa Chadema taifa; Paul Joseph, Afisa wa Chadema, Kanda ya Nyasa; Kelvinn Ndadibila, Afisa Habari Kanda ya Nyasa, Michael Msongole, mwenyekiti wa Chadema, wilaya ya Mbozi, walinzi wa Mbowe – Mohamed Ling’wanya na Halfani Bwire – pamoja na Ezekia Zamzbi, mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, mkoa wa Songwe.

Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi, viongozi hao wa chama kikuu cha upinzani nchini, wamekamatwa baada ya kufanya vurugu kwenye eneo la stendi ya zamani ya Mlowo, wlayani Mbozi, kufuatia hatua ya Chadema, kutaka kufanya mkutano wa kampeni eneo ambalo hawakustahili.

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema

“Chadema walitaka kufanya kampeni eneo ambalo halikustahili. Ndipo askari walipowapa amri ya kutawanyika. Lakini wakakaidi. Ndipo askari waliamua kuwatawanya kwa nguvu na dipo walipoanza kurusha mawe…”.

Imeongeza: “Katika tukio hilo, askari wawili wamejeruhusiwa maeneo ya kichwani, usoni na puani na kwa sasa wanaendelea na matibabu hosptali ya wilaya ya Mbozi.”

Katika taarifa hiyo, jeshi hilo, limewataka viongozi wa vyama vyote kutii na kufuata walichoita, “ratiba zilizotolewa na Wasimamizi wa Uchaguzi, ili kuepusha vurugu zinazoepukika.

About The Author