November 17, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Waliokufa ajali K’koo wafikia 13, Rais aagiza uchunguzi ufanyike

 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema kuwa, Serikali itabeba gharama za matibabu kwa majeruhi wote walionusulika kwenye ajali ya kuporomoka kwa ghorofa K/koo jiijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Rio de Janeiro, Brazil … (endelea).

Ghorofa hilo limeporomoka jana tarehe 16 Novemba 2024, majira ya Asubuhi, kwenye mtaa wa Congo na Mchikichi huku chanzo chake mpaka sasa kikiwa hakijaelezwa.

Akizungumza ma watanzania akiwa nchini Brazil, Rais Samia amesema kiwa, katika ajali watu 84 wameshaokolewa mpaka saa nne ya leo asubuhi, huku watu 13 wakiwa wamepoteza maisha.

Baadhi ya watu ambao wameokolewa baada ya kufukiwa na vifusi, walifikishwa hospital na baadhi kuruhusiwa, huku wengine 26 wakiendelea na matibabu mbalimbali.

Aidha Rais Samia aliongezea kuwa, Serikali itabeba gharama zote za matibabu kwa majeruhi wote, na itahakikisha waliopoteza maisha wanastiliwa.

“Serikali itabeba gharama za matibabu kwa majeruhi wote na itahakikisha waliopoteza maisha wanastilia, nitoe pole kwa ndugu, jamaa na marafiki walioguswa na tukio hili.” Alisema Rais Samia.

Katika hatua nyingine Rais Samia alimuagiza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, angoze timu ya wakaguzi majengo kugagua eneo lote la K/koo na kupata taarifa kamili ya hali ya majengo ya K/koo yalivyo.

Lakini pia Rais Samia alitoa maagizo kwa jeshi la Polisi, kupata taarifa kamili kwa mmliki wa jengo lililoporomoka jinsi ilivyokuwa wakati wa ujenzi.

About The Author