January 22, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Nani kuibuka mshindi? Mike Tyson na Jake Paul

 

Leo litapigwa pambano la kibabe la masumbwi ambapo bingwa wa zamani wa dunia uzito wa juu Mike Tyson atapigana bondia Jake Paul kwenye pambano ambalo linasubiriwa kwa hamu sana.

Bondia Mike Tyson maarufu kama Iron Mike ambaye alikua bingwa wa dunia uzito wa juu mwenye asilimia 88% za ushindi kwenye mapambano yake ambapo alishinda mapambano 50 kwenye mapambano 58 rasmi aliyopigana.

Pambano hili sio rasmi lakini limeonekana kuvuta hisia za watu wengi kutokana na ubora ambao alikua nao Mike Tyson, Lakini pia umaarufu ambao amejizoelea Jake Paul za hivi karibuni kwani kijana huyo mwenye umri wa miaka 27 amekua moja ya watu wanaofatiliwa zaidi kwenye mtandao wa You Tube.

Jake Paul ni kijana wa miaka 27 ambaye alianza kwa kutengeneza maudhui kwenye mtandao wa You Tube mwaka 2014 kabla ya kugeukia kwenye masumbwi mwaka 2018, Ambapo alifanikiwa kupigana mapambano kadhaa na kufanikiwa kushinda na mengine kupoteza.

Kijana huyo wa miaka 27 amekua moja ya wanamichezo maarufu kwani aliwahi kutajwa na jarida la Forbes kama kijana ambaye analipwa zaidi wakati akitengeneza maudhui kwenye mtandao wa You Tube, Jambo ambalo limemfanya aendelee kua na thamani hata pale ambapo aligeukia kwenye masumbwi.

Pambano la Mike Tyson na Jake Paul lilitarajiwa kufanyika mwezi Julai 20 mwaka huu, Lakini kutokana na bondia Mike Tyson kua na matatizo ya kiafya ndio pambano likasogezwa mbele na kutarajiwa kupigwa leo Novemba 15.

Endelea kufurahia kubashiri na Meridianbet mabingwa wa michezo ya kubashiri ambao wanatoa ODDS BOMBA kuliko mahala pengine, Lakini pia machaguzi mengi zaidi ya 1000 Bashiri sasa michezo itakayopigwa wikiendi hii uweze kupiga mkwanja.

Jambo la kufurahisha kuhusiana na pambano hilo tofauti ya umri uliopo baina ya Mike Tyson na Jake Paul ambapo wameachana umri wa takribani miaka 31 kwani Mike Tyson ana miaka 58 huku Jake Paul akiwa ana miaka 27.

Licha ya kua pambano hili sio rasmi na halitakua na mkanda lakini limevuta hisia za watu na kulisubiri kwa hamu kutokana na ubora ambao Mike Tyson alikua nao miaka ya nyuma, Lakini pia Jake Paul ambaye amekua akivutia watu wengi kutokana na maudhui yake.

About The Author

error: Content is protected !!