November 21, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Chadema, Lissu wavutana, wajibu hoja zake

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti Chadema Bara

 

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, imetoa ufafanuzi kuhusu hoja mbalimbali zilizotolewa hivi karibuni na Makamu Mwenyekiti Bara wa Chama hiko Tundu Lissu katika mikutano yake mbalimbali na wanahabari. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Katika taarifa kwa umma, iliyotolewa hii leo tarehe 14 Novemba 2024, chama hiko kimeeleza kuwa hakijawahi kuletewa hoja ya kugawana madaraka na chama chochote au hoja ya kupewa majimbo ya uchaguzi na nafasi za kugawana madaraka muundo wa Serikali.

Hoja hiyo ilibuliwa hivi karibuni na Tundu Lissu, akisema ya kuwa chama hiko kilidanganywa kwenye kile kilichoitwa maridhiano dhidi ya CCM, kwa kuahidiwa baadhi ya nafasi za uongozi kwenye Serikali ikiwemo nafasi ya uwaziri Mkuu na Umakamu wa Rais.

Chama hiko kimetoa ufafanuzi ya kuwa, nafasi ya umakamu wa Rais ni ya kugombewa na haitolewi mezani kwa mujibu wa katiba ya nchi kwa sasa, aidha taarifa hiyo iliendelea kueleza kuwa hata nafasi ya Uwaziri Mkuu haitolewi mezani bali ni kutokana na chama chenye wabunge wengi bungeni kama ilivyo kwa mujibu wa katiba.

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema

Taarifa hiyo iliendelea kueleza kuwa, Chama hiko kupitia vikao vyake rasmi, hakijawahi kujadili, kutoa au kupokea mapendekezo yeyote ya kitu kinachoitwa ‘nusu mkate’ kama ilivyotolewa na Lissu kwenye mkutano wake na waandishi wa Habari hivyo karibuni mkoa Singida.

Kuhusu maridhiano Chadema imesema kuwa vikao hivyo vya maridhiano, vilihitimishwa rasmi tarehe 03 Novemba 2024, na baada ya hapo hakuna kikao chochote cha siri kilichofanyika hivi karibuni kati ya Chadema na CCM.

Wakijibu Kuhusu tuhuma dhidi ya Fedha chafu au rushwa, Chadema wamefafanua kuwa, tuhuma hizo zilikuwepo kwa baadhi ya maeneo lakini zimekosa vielelezo vya ushaidi wa kisheria na maeneo mengine uchunguzi wa ndani unaendelea.

Kufuatia ufafanuzi huo, Chadema imetoa rai kwa wanachama wao kuwekeza nguvu kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa na kupuuza propaganda za kuigawa chama, uchaguzi huo unatarajia kufanyika tarehe 27 Novemba 2024.

About The Author