November 12, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

DC Nassari afyungua Kongamano la Wafanyabiashara wilayani Magu

Mkuu wa Wilaya ya Magu, Joshua Nassari

 

MKUU wa Wilaya ya Magu, Joshua Nassari amesema Serikali inatambua mchango wa wafanyabiashara wilayani humo katika kukuza uchumi wa wilaya na nchi kwa ujumla. Anaripoti Mwandishi Wetu, Magu, Mwanza … (endelea).

DC Nassari ameyasema hayo wakati akifungua kongamano la wafanyabiashara Wilayani Magu lilofanyika Novemba 07,2024 katika ukumbi wa CCM Magu ambapo alibainisha kuwa serikali itaendelea kushirikiana na wafanyabiashara.

DC Nassari amesema serikali inatambua mchango wa sekta ya biashara kwani imekuwa mstari wa mbele katika kutoa ajira kwa vijana na kukupa uchumi kupitia kodi mbalimbali wanazitoa serikalini ambazo zinasaidia kukuza uchumi.

Aidha, DC Nassari ametoa rai kwa wafanyabiashara Wilayani Magu kuchangamkia fursa ya kushiriki makongamano mbalimbali kwani yanasaidia kuwakutanisha wafanyabiashara pamoja na kuwasilisha kero zao kwa serikali kwaajili ya utatuzi.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu Mohamed Ramadhani amewataka wafanyabiashara wazawa kujiunga na mfumo wa kielektroniki wa ununuzi wa umma ( NEST) ili kupata zabuni zinazotolewa na serikali na kufanikiwa kwa kukuza pato mtu mmoja na Taifa kwa ujumla.

Amesema mfumo huo unawalinda wafanyabiashara na unatenda haki wakati wa kutangaza zabuni na hakuna upendeleo wowote wakati kutangaza tenda huku akiwataka wafanyabiashara kuweka bei Rafiki zinazoendana na soko.

Baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria kongamano hilo akiwemo Suzy Shija ambaye ni msindikaji na mchakataji wa bidhaa wameishukuru Halmashauri kwa kuandaa kongamano hilo kwani limesadia wafanyabiashara kupata elimu na kuwasilisha kero zao kwa uongozi na baadhi ya kero zimetatuliwa wakati wa kongamano.

About The Author