December 23, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Ushirikishwaji wa wanawake na wenye ulemavu wasisitizwa kuongeza Maendeleo

 

KAMPUNI ya Serengeti Breweries Limited (SBL) imezindua rasmi Ripoti yake ya Uendelevu ya 2024 yenye kauli mbiu Kusimamia Ujumuishwaji na Ushirikishwaji, mnamo Oktoba31, 2024. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Ripoti hii inaangazia dhamira ya SBL ya kuendeleza mazingirajumuishi ambapo watu wenye asili mbalimbali wanaweza kufanikiwa, kwakuzingatia kuondoa vikwazo na kuleta athari chanya kwa jamii, wasambazaji, na wadau.

SBL, ikifanya kazi chini ya East African Breweries Limited (EABL), imepangakutenga rasilimali za kutosha kuwekeza katika jamii kupitia mpango wao waSpirit of Progressmpango wa ESG unaolenga kuunda jamii endelevu katikamaeneo wanayoyahudumia. Tukio hilo liliwakutanisha mamia ya wadau nakufanya mazungumzo kuhusu namna ya kuboresha ushirikiano ili kuendelezausawa wa kijinsia na uwezeshaji wa kiuchumi kwa kushughulikia changamoto, fursa, na uboreshaji wa sera.

Shabnam Mallick, Mkuu wa Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa(UN), alihudhuria tukio hilo na kutoa mtazamo wake, akisisitiza umuhimu waushirikiano, uboreshaji wa sera, na hatua za pamoja katika kuendeleza usawawa kijinsia kama nguzo ya uwezeshaji kiuchumi na uendelevu katika taasisiyoyote.

 

 

Ninafurahi kuona hatua kubwa ambazo SBL imepiga katika kukuza usawa wakijinsia na kuunga mkono wanawake katika nafasi za uongozi. Ninafurahia pia kuona kwamba kampuni imeweka malengo ya matumizi kwa wasambazajimbalimbali pamoja na ufuatiliaji. Hiki ni kitendo cha makusudi ambacho nimuhimu katika kufikia malengo yetu ya muda mrefu ya uendelevu nakuhakikisha maendeleo yanawafikia wote, alisema Mallick.

Mwenyekiti wa Bodi ya SBL, Paul Makanza alikazia mbinu zinazotumikakuhakikisha ripoti za uendelevu zinakuwa chachu ya maendeleo kiuchumiAfrika, alisema, Wanawake wanapokuwa na fursa sawa, uchumi unakua, familia zinastawi, na jamii zinaendelea. Tukifunga pengo la kijinsia barani Afrika, inaweza kuongeza dola bilioni 316 kwenye uchumi wetu kufikia mwaka2025. Huo ndio ukuaji. Na hii ni sehemu ambayo SBL tumedhamiria kuhusikazaidi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Obinna Anyalebechi, alizungumziamchango wa kampuni yao kwenye ukuaji jumuishi na uwezeshaji kiuchumi wamakundi maalum nchini, akisema, Juhudi zetu za ushirikishwaji na usawazinaakisi dhamira yetu ya kuwezesha makundi yaliyotengwa, ikiwa ni pamojana wanawake, watoto, na watu wenye ulemavu, ili wafaidike na fursa za kijamiina kiuchumi.

“Najivunia kuripoti kwamba karibu asilimia 40 ya wakulimatuliowawezesha mwaka huu walikuwa ni wanawake na watu wenye ulemavuambao wanalima mtama, moja ya viungo muhimu katika uzalishaji wa bia zetu. Kupitia ushirikiano wetu na Sightsavers, tumewaunga mkono zaidi yawanawake na watu wenye ulemavu 200 katika mkoa wa Singida, tukiwasaidiakukuza mtama kwa ajili ya uzalishaji kwa SBL,” alisema Anyalebechi.

Ripoti hii inaeleza zaidi mipango ya kimkakati ya SBL inayolenga kuondoavikwazo vinavyozuia ushirikishwaji na maendeleo, hasa kwa wanawake nawatu wenye ulemavu. Mipango hii, ambayo inaambatana na ahadi kubwa za ESG za SBL, inachangia kwa kiasi kikubwa Malengo ya Maendeleo Endelevuya Umoja wa Mataifa (SDGs).

SBL imeendelea kusisitiza nia yake ya kuimarisha juhudi zake za uendelevu ilikuleta athari chanya katika jamii nchini kwa kupitia ushirikiano na washirika, wadau, na jamii kwa ujumla, kuhamasisha mazingira bora ambapo ushirikishina uwezeshaji kiuchumi ni muhimu katika maendeleo.

About The Author

error: Content is protected !!