BUNGE la Seneti limethibitisha kukumbana na matatizo ya kiufundi na mfumo wao wa barua pepe, kufuatia wimbi la mawasilisho yaliyotolewa na Wakenya kuhusu muswada wa Katiba ya Kenya (Marekebisho) (Nambari 2), wa 2024. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa, Nairobi, Kenya … (endelea).
Muswada huo, uliowasilishwa na seneta wa Nandi, Samson Cherargei, unalenga kuongeza ukomo wa muhula wa Rais, magavana, wabunge wa bunge la taifa na wabunge wa mabunge ya kaunti kutoka miaka mitano ya sasa hadi saba.
Awamu ya ushirikishwaji wa umma wa muswada huo, ilitarajiwa kukamilika leo tarehe 25 Oktoba, huku Wakenya wakihimizwa kutoa maoni yao kwa mkono katika Ofisi ya Karani wa Seneti, au kwa barua pepe.
Muswada huo umekosolewa na wananchi wengi ambao wameeleza kusikitishwa na mtazamo wa serikali, kutosikiliza maoni ya wananchi wanaopinga nyongeza ya muda kwa viongozi wa kuchaguliwa.
Seneti limesema mfumo wao wa barua pepe umepokea zaidi ya mawasilisho 200,000 na kufikia upeo wa juu wa anwani za barua pepe.
Hayo yanatokea wakati ambao leo, Kamati ya Bunge la Seneti nchi Kenya, ikipokea maoni ya umma kuhusu muswada huo, unaolenga kuongeza ukomo wa muda wa madarakani kwa viongozi waliochaguliwa kutoka miaka mitano hadi saba.
Kamati ya haki na masuala ya sheria, imepokea maoni ya wananchi, mengi yakionesha kuukosoa vikali.
Seneta Samson Cherargei, aliyewasilisha muswada huo anatokea Bonde la Ufa, eneo ambalo ni ngome ya Rais William Ruto.
ZINAZOFANANA
Ukraine wakiri kufanya mauaji ya Jenerali wa Urusi na msaidizi wake mjini Moscow
Lungu akwama kuwania urais Zambia
Wananchi Comoro wafurahia huduma madaktari wakitanzania