November 21, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Papa Potwe ni alama mpya inayoitambulisha Tanzania kwenye ramani ya Dunia

 

WAKATI Afrika Kusini bendera yao inapepea dunia kwa kuwa na kivutio cha kipekee cha Kifaru mweupe Tanzania kwenye visiwa vya Mafia yupo Papa Potwe kwa kiingereza Whale Shark, watalii hutoka sehemu mbalimbali duniani kumfuata Potwe. Anaripoti Faki Sosi, Mafia … (endelea).

Hatujamtanga vizuri, siku tukiamua kumtangaza tutakuwa hatuana hoteli za kuwaweka wageni watakaovutiwa na habari zake. leo kwa uchache sana nimeona niseme juu ya kivutio hiki muhimu na adimu kilichopo nchini mwetu.

Papa Potwe, anayejulikana pia kama “Whale Shark,” ni samaki mkubwa wa baharini anayepatikana katika maji ya joto duniani sehemu chache duniani, ikiwa ni pamoja na pwani za Tanzania katika Kisiwa cha Mafia. Aina hii ya samaki imekuwa kivutio kikubwa cha watalii kutoka sehemu mbalimbali za dunia, na sasa inachukuliwa kuwa alama muhimu ya utalii nchini Tanzania.

Makala hii inachunguza kwa undani jinsi Papa Potwe alivyojipatia sifa kama alama ya kivutio cha utalii nchini Tanzania na umuhimu wake kwa uchumi wa taifa.Samaki Potwe: Alama Mpya ya Kivutio cha Utalii Tanzania , Tanzania ni maarufu kwa vivutio vyake vya utalii, kama vile Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, na Ziwa Victoria. Hivi karibuni, samaki Potwe ameongezeka umaarufu na kuwa miongoni mwa vivutio vya pekee ambavyo vimevutia wageni wengi kuja nchini. Samaki Potwe amegeuka kuwa alama ya kipekee katika sekta ya utalii, hususan katika maeneo ya pwani ya Tanzania Bara.

Kipekee Potwe anapatika katika Kisiwa cha Mafia pekee pamoja na kuwa kipo kusini mwa Jiji la Dar es Salaam kwa umbali wa Kilometa 195, ambapo kwa upande wa Kaskazini kisiwa hiki kipo karibu zaidi na Wilaya ya Mkuranga, upande wa Kusini Magharibi Rufiji na Kilwa huku Kusini Magharibi ni bahari ya hindi na kimsingi kisiwa hiki kimezungukwa na bahari ya Hindi.

Kwa maeneo yote yaliyokaribu na kisiwa hicho hajawahi kuonekana huyu Papa Potwe baadhi ya watu wa Mafia husema samaki huyo hupenda kuishi maeneo ya Mafia kwa kuwa kuna utulivu zaidi kwake.

Maajabu yake

Papa Potwe anaweza kufika urefu wa mita 18.4 urefu wake huongezeka kulingana na umri wake akiwa na miaka 20 anakuwa na urefu wa mita 5. Wataalamu wa uhifadhi husema kuwa Papa Potwe wenye mita 6 wenye umri wa mdogo zaidi ndio huonekana zaidi kisiwani Mafia. Inaelezwa kuwa sehemu nyingine duaniani ambazo Papa Potwe huonekana ni huenekana hawa wadogo wa mita 5 hadi sita (Ukienda Afrika Kusini, Seychelles, wala sio Australia.

Rafiki yangu Juma Salumu mtaalamu wa mambo ya uhifadhi pia Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia, ameandika kuwa majina yao ambayo waongoza watalii na wamewapa ili kutambulika.

Mathalani, Santa-TZ009 huyu Potwe dume mwenye mita 7 mwenye alama ya kovu kubwa katika pezi lake la Juu , ndani ya miaka 16 alionekana mara 58 ambapo tarehe 30 Oktoba 2010 alionekana Seychelles huku tarehe 7 Disemba 2012 alirudi viwanja vya nyumabni kisiwani Mafia na kuungana na wenzie kina Hamis (TZ-090), Casper , Rocky, Chambo, Butterfly , Kadar na Tina (TZ-136).

Umuhimu wa Samaki Potwe kwa Utalii

Kivutio kwa Watalii: Samaki Potwe ni miongoni mwa samaki wakubwa zaidi duniani, na uwepo wake unawapa watalii nafasi ya kipekee ya kuwaona na hata kuogelea nao. Hii imewavutia watalii wengi kutoka pande mbalimbali za dunia kuja Tanzania kwa ajili ya uzoefu huu wa aina yake.

Kuongezeka kwa Mapato ya Utalii: Utalii unaohusisha samaki Potwe umeleta mchango mkubwa katika uchumi wa maeneo husika. Hoteli, huduma za usafiri wa baharini, na biashara nyingine zinazohusiana na utalii zimeweza kukuza uchumi wa maeneo ya pwani kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watalii.

Kuongeza uhamasishaji wa uhifadhi wa mazingira: Kivutio hiki kimechangia kuongeza uhamasishaji juu ya umuhimu wa uhifadhi wa mazingira ya baharini. Serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali wameanzisha miradi mbalimbali ya kuhifadhi mazingira ya baharini ili kuhakikisha uwepo wa samaki hawa kwa muda mrefu.

Mabadiliko ya Tabianchi: Mabadiliko ya hali ya hewa yanayoathiri joto la bahari yanaweza kuathiri makazi ya samaki Potwe na kuathiri idadi yao. Uchafuzi wa Mazingira ya Baharini: Uchafuzi wa bahari kwa plastiki na kemikali ni changamoto nyingine inayohatarisha maisha ya samaki Potwe, hivyo kufanya uhifadhi wao kuwa muhimu zaidi.

Samaki Potwe si tu kwamba ni mnyama mkubwa wa baharini, bali pia amegeuka kuwa alama muhimu ya utalii wa Tanzania. Kwa kuwa kivutio kikubwa cha watalii na chanzo cha mapato kwa taifa, ni muhimu kuwekeza katika uhifadhi wa samaki hawa ili kuhakikisha wanabaki kuwa sehemu ya urithi wa taifa kwa vizazi vijavyo. Mikakati ya uhifadhi inapaswa kuendelezwa na kuimarishwa ili kulinda urithi huu wa pekee, na kuendelea kuvutia watalii kutoka kote duniani.

About The Author