MKURUGENZI wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Kailima Ramadhani amejiandikisha kwenye daftari la wakazi katika mtaa wa Chimuli II kwenye kituo cha Shule ya Msingi Chadulu jijini Dodoma leo Oktoba 19, 2024. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Akizungumza baada ya kujiandikisha, Kailima aliwasisitiza wananchi umuhimu wa kujitokeza kwa wingi kuandikishwa katika maeneo yao ili watimize haki yao ya kikatiba ya kupiga kura.
“Nimetoka kujiandikisha katika orodha ya wakazi ambayo itazaa daftarinla orodha ya wapiga kura kwaajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa, niwaombe na kuwasihi wananchi wote wenye umri wa miaka 18 na wenye sifa za kuandikishwa wajitokeze kuandikishwa ili watumie haki yao ya kikatiba ya kupiga kura.
Kailima amesema watu wa makundi yote, Wazee, wakina mama na vijana wenye sifa wajitokeze kwani imesalia siku moja ili kuhitimisha zoezi hilo kwaajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa.
Aidha amesema vituo vipo katika maeneo mbalimbali yaliyo karibu na makazi ya wananchi hasa katika mashule na ofisi za mitaa.
Uandikishaji wa wapiga kura wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, kwenye daftari la wakaazi, ulianza tarehe 11 Oktoba, 2024 na utamalizika tarehe 20 Oktoba 2024.
Wananchi waliojiandikisha watapiga kura kuchagua viongozi wa mitaa na vijiji tarehe 27 Novemba, 2024 katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
ZINAZOFANANA
Wagombea wasioridhishwa na uteuzi waweke pingamizi
Mluya awachimba mikwara wasimamizi wa uchaguzi “atakavuruga tutashughulika naye’’
Wajumbe wa CCM Dodoma wamkataa mgombea aliyeteuliwa