As Monaco wanakimbiza mwizi kimya kimya ndio kauli ambayo unaweza kuitumia kwa klabu hiyo ambayo mpaka sasa ndio vinara wa ligi kuu nchini Ufaransa maarufu kama Ligue 1.
Klabu ya As Monaco katika hali ya kushtusha wamefanikiwa kushika usukani wa ligi kuu ya soka nchini Ufaransa baada ya michezo saba ya ligi hiyo kuchezwa, Huku wakiwa wakifanikiwa kushinda michezo sita na kusuluhu mmoja wakiwa hawajapoteza mchezo.
Monaco mpaka sasa wana jumla ya alama 19 kwenye msimamo wa ligi hiyo huku wakionesha ubora mkubwa kwenye michezo yao ambayo wamecheza msimu huu, Hii ikitoa mwanga mzuri kua huenda msimu huu klabu hiyo ikafanya jambo kubwa baada ya muda mrefu ya kutokua kwenye ubora wao.
Klabu hiyo licha ya kua haijakutana na vigogo kadhaa wa ligi hiyo kama PSG, Olympique Marseille, pamoja na Lille lakini wamekua wakitandaza soka safi kweli chini ya kocha Adi Hutter kwani hata kwenye michuano ya ulaya wameanza vizuri msimu.
Endelea kufurahia kubashiri na Meridianbet mabingwa wa michezo ya kubashiri ambao wanatoa ODDS BOMBA kuliko mahala pengine, Lakini pia machaguzi mengi zaidi ya 1000 Bashiri sasa michezo itakayopigwa wikiendi hii uweze kupiga mkwanja.
Klabu ya PSG mabingwa watetezi wa ligi hiyo nao hawapo mbali kwenye msimamo kwani wanawafukuza Monaco, Ambapo wao wanakamata nafasi ya pili wakiwa na alama 17 wakicheza michezo 7 na kushinda michezo mitano huku wakisuluhu michezo miwili.
ZINAZOFANANA
Piga mkwanja Jumapili ya leo kupitia Ligi mbalimbali barani Ulaya
Teleza na ODDS za Meridianbet Jumamosi hii
Bashiri na Meridianbet mechi za leo