December 24, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

TRA yazindua ofisi ya walipa kodi binafsi

 

MAMLAKA ya Mapato Tanzania(TRA) imezindua ofisi ya walipa kodi binafsi na wenye hadhi ya juu 158 ilikuongeza ufanisi wa ukusanyaji mapato. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Yusuph Mwenda amezindua ofisi hiyo dar es salaam Oktoba 15,2024 .

“Muunganiko huu na matokeo haya ni kutokana na muundo mpya uliotengenezwa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ambapo ofisi hii itakuwa ikihudumia makundi manne ambayo ni wamiliki wa makampuni makubwa yanayozalisha zaidi ya shilingi bilioni 20 kwa mwaka.

Makundi mengine ni wamiliki wa hisa zenye thamani ya shilingi bilioni 2.5 kwa mwaka,wale wote wenye ubia kwenye makampuni yanayozalisha zaidi ya shilingi bilioni 20, viongozi wa mihimili mitatu pamoja na taasisi binafsi walioteuliwa wote watahudumiwa na ofisi hii na ni asilimia 30 tu ya mapato watakayochangia,”amesema Mwenda.

Mwenda amesema sababu kubwa ya kuanzishwa kwa ofisi hiyo ni kutokana na mchango mkubwa unaotolewa na makundi hayo kwani kushindwa kuyapa huduma stahiki kutasababisha serikali kupoteza mapato na kufanya uchumi wa nchi kushuka.

Amesema Mamlaka imeanza na idadi hiyo kwani ndio waliokidhi vigezo vya kuhudumiwa katika ofisi hiyo.

“Katika makundi yaliyoainishwa walipaji kodi binafsi waliokidhi vigezo na kupata sifa ni 111 huku viongozi kutoka mihimili mitatu na taasisi wakiwa 47 hivyo ni lazima watu hawa tuwenao karibu ilikuwapa elimu zaidi waweze kulipa kile wanachostahili,”amesema Mkenda.

Amesema mamlaka inahitaji kuweka na kuleta usawa katika usimamizi na ulipaji wa kodi kwani watu hawa walikuwa wanalipa kodi lakini si kwa usahihi sababu makundi waliyokuwepo hayakuwa sahihi pia hata huduma walizokuwa wakipewa huko hazikuwa rafiki kwani kuna watu walikuwa kundi la walipa kodi wakubwa, wakati na walipa kodi wadogo sasa tunawaleta pamoja ili kuweza kutafasiri sheria za kodi.

Naibu Kamishina Mkuu wa mamlaka hiyo, Mcha Hassan Mcha amesema ufunguzi wa ofisi hiyo ni kuongeza huduma na kuongeza ufanisi wa kazi ilikusaidia kuwatambua walipa kodi wote na kufahamu zaidi namna ya ulipaji,ili kuongeza uweledi wa ukusanyaji mapato na kuongeza walipa kodi kwa hiari na kuwahudumia bila changamoto.

About The Author

error: Content is protected !!