HALMASHAURI ya Wilaya ya Karatu, mkoani Arusha imetenga Sh. 1.1 bilioni, kwa ajili ya mikopo ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwa mwaka 2024/2025. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Juma Hokororo, amewaambia wanahabari leo tarehe 01 Oktoba 2024, kuwa kati ya fedha hizo, Sh. 440 milioni zimetengwa kwa ajili ya wanawake, Sh. 440 milioni kwa ajili ya vijana na Sh. 220 milioni kwa ajili ya watu wenye ulemavu kwenye Halmshauri hiyo.
Hokororo amesema sifa za makundi hayo kunufaika na fedha hizo ni sharti awe Mtanzania mwenye miaka kuanzia 18, mwenye akili timamu, aliye kwenye vikundi vilivyosajiliwa na kuwa na watu kuanzia watano na vikundi hivyo pia viwe vina akaunti kwenye Benki mbalimbali huku wajumbe pia wakitakiwa kutokuwa na ajira rasmi.
Serikali ilisitisha utoaji wa mikopo hiyo kwa muda, ili kuandaa utaratibu mzuri zaidi wa utoaji wa mikopo hiyo.
Hokororo amewaambia wananchi kuwa kutokana na maboresho yaliyofanyika, mchakato mzima wa uombaji na upataji wa mikopo umerahisishwa na utatumia muda mfupi zaidi.
ZINAZOFANANA
Serikali yaipa ITA jukumu la utafiti wa mapato
Benki ya NBC yatambulisha kampeni ya Kilimo Mahususi kwa wakulima na wafugaji Mbeya
Upelelezi wakwamisha kesi ya Boni Yai