October 13, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

NBC yakabidhi tuzo, fedha kwa mchezaji na kocha bora Agosti

 

BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC), mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu ya NBC jana Alhamisi iliipamba mechi kati ya Azam FC na Simba SC maarufu kama ‘Mzizima Derby’ kwa kuandaa matukio kadhaa ikiwemo kukabidhi zawadi ya tuzo na pesa taslimu kwa mchezaji na kocha bora wa ligi hiyo kwa mwezi Agosti. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Katika mechi hiyo iliyofanyika kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar na kuisha kwa timu ya Simba SC kuibuka na ushindi wa goli 2-0, washindi wa droo mbalimbali zinazoandaliwa na benki ya NBC walipata fursa ya kuutazama mchezo huo wakiwa katika jukwaa la VIP kupitia udhamini wa benki hiyo.

Meneja wa Benki ya NBC tawi la Zanzibar Bw Abdul Karim Mkila aliiwakilisha benki hiyo katika kukabidhi tuzo na hundi ya fedha yenye thamani ya sh mil 1, kwa mchezaji bora mwezi Agosti, ambae ni kiungo wa Simba SC, Jean Charles Ahoua huku Mwenyekiti wa Chama Cha Soka Mkoa wa Dar Es Salaam (DRFA) Lameck Nyambaya akikabidhi zawadi kama hizo kwa kocha mkuu wa klabu ya SC Fadlu Davids ambae pia aliiibuka kocha bora kwa mwezi huo.

Katika mchezo huo wa jana pia ilishuhudiwa kipa wa Simba SC, Moussa Camara akiibuka mchezaji bora wa mchezo huo na kukabidhiwa zawadi ya tuzo kutoka benki hiyo.

About The Author