September 19, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Ulaya yakumbwa na maafa ya mafuriko

 

MVUA kubwa zilizoanza kunyesha Alhamisi iliyopita, zimesababisha mafuriko, vifo na kulazimisha watu kuyakimbia makazi yao, katika nchi nne za Ulaya. Prague, Czech

Vyombo vya habari vya kimataifa vimeripoti kuwa nchi zilizokumbwa na mafuriko ni Austria, Jamhuri ya Czech, Poland na Romania, huku Slovakia na Hungary zikitarajiwa kujiunga kwenye orodha hiyo kutokana mvua kubwa zinazondelea kunyesha.

Vimeripoti kwamba, tayari watu sita wamethibitishwa kupoteza maisha nchini Romania, mmoja Austria na mwingine Poland.

Ripoti ya polisi imeeleza kuwa nchini Jamhuri ya Czech, watu wanne hawajulikani walipo baada ya kusombwa na mafuriko na kwamba Jamhuri ya Czech imeathiriwa zaidi huku mamlaka nchini humo ikitangaza hali ya tahadhari katika zaidi ya sehemu 100.

Kwenye mji wa Opava, takribani watu 10,000 kati ya jumla ya watu 56,000 wameombwa kuhamia kwenye maeneo salama ya nyanda za juu, waokoaji walitumia boti kuwasafirisha, kutokana na kufurika kwa mto Opava.

About The Author