RAIS wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, amesema kwamba taifa hilo halina silaha zinazoweza kuwatosheleza wanajeshi wake. Kyiv, Ukraine.
Akizungumza jana Jumapili, Rais Zelensky alisema kwamba Ukraine inahitaji kuzipatia silaha brigedi 14, lakini uwezo wake ni brigedi 4 pekee.
Zelensky alimwambia mwandishi wa habari wa Marekani, Fareed Zacharia kwenye mahoajiano ambayo pia yalichapishwa kwenye mtandao wa Telegram na vyombo vya habari vya Ukraine.
Zelensky amesema Ukraine imetumia akiba yake yote na hasa wakati Bunge la Marekani lilipozuia upelekwaji wa silaha na kusisitiza kwamba ni lazima hifadhi yake iwe na silaha tena.
ZINAZOFANANA
Wananchi Comoro wafurahia huduma madaktari wakitanzania
Chama cha upinzani Namibia chaomba zoezi la kuhesabu kura lisitishwe
Ushiriki wa Rais Samia G20 wainufaisha Tanzania