MAHAKAMA ya kijeshi nchini Congo (DRC), imewahukumu adhabu ya kifo watu 37, wakiwemo Wamarekani watatu, baada ya kuwatia hatiani kwa mashtaka ya kushirki katika jaribio la mapinduzi. Anaripoti Mwandishi Wetu kwa msaada wa DW.
Washtakiwa hao, wengi wao wakiwa raia wa taifa hilo, lakini wakiwemo pia Muingereza, Mbelgiji na Mcanada, wana muda wa siku tano kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.
Mbali na mashitaka hayo, washitakiwa walikabiliwa na mashtaka ya ugaidi na ushirika wa uhalifu.
Watu 14 wameachiwa huru katika kesi hiyo iliyoanza mwezi Juni.
Watu sita waliuawa wakati wa jaribio hilo lililoongonzwa na mpinzani asiemaarufu Christian Malanga mnamo mwezi Mei, ambalo lililenga kasri la rais na mshirika wa karibu wa rais Felix Tshisekedi.
Malaga aliuawa katika ufyatulianaji risasi na vikosi vya usalama vilipojaribu kumkamata, na mtoto wake Marcel Malanga, ambaye ni raia wa Marekani mwenye umri wa miaka 21 ni miongoni mwa waliohukumiwa kifo.
ZINAZOFANANA
Samia kutikisa Brazil mkutano wa wakuu wa kundi la G20
Waziri Kijaji afanya mazungumzo na wadau wa COP29
Korea Kusini lawamani kukandamiza uhuru wa dini