September 19, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Mkalama yatangaza mkakati wa kupambana na Homa ya Nyani

 

MKUU wa wilaya ya Mkalama, Moses Machali amewataka Wakuu wa Idara, Watumishi wa Afya, Watendaji Kata na Vijiji pamoja na Maafisa Tarafa wilayani Mkalama kutoa elimu kwa wananchi namna ya kujilinda na ugonjwa wa Homa ya Nyani maarufu kama Mpox. Anaripoti Mwandishi Wetu, Singida … (endelea).

Wito huo ameutoa leo tarehe 5 Septemba, 2024 wakati wa kikao cha afya ya msingi wilayani Mkalama kilichofanyika kwenye ukumbi ulipo ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mkalama.

“Wakuu wa Idara, watumishi wa afya, Watendaji kata na Vijiji pamoja na Maafisa Tarafa kwa pamoja twendeni tukaelimishe jamii kuhusu homa ya nyani na namna ya kujilinda na ugonjwa huu,” alisema Machali.

Aidha, katika kuhakikisha wananchi wanajilinda na ugonjwa huo, Machali amepiga marufuku wananchi kusalimiana kwa kupeana mikono ili kujilinda na ugonjwa huo.

“Kuanzia leo tusisalimiane kwa kupeana mikono, tukifanya hivi tutajilinda na sisi na kuwalinda wengine,” amesema Machali.

Vile vile, Machali ametoa agizo kuwekwa maji yanayotiririka pamoja na sabuni katika maeneo yote ya taasisi za umma pamoja na yale yenye watu wengi.

Awali akiwasilisha hali ya ugonjwa huo, Afisa Afya Wilaya ya Mkalama, Dorice Damiani amesema kuwa ugonjwa huo unaambukizwa kwa njia mbalimbali ikiwemo kushikana mikono, kujamiana na mtu mwenye ugonjwa huo pamoja na kuchangiana nguo.

 

About The Author