September 20, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Baraza la vyama lataka wasimamizi wafundwe wasiharibu uchaguzi

BARAZA la Vyama vya Siasa Tanzania, limetaka wasimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wapewe mafunzo ili wausimamie vizuri kwa ajili ya kuenzi maono ya Rais Samia Suluhu Hassan, ya kuleta maridhiano ya kisiasa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Wito huo umetolewa hivi karibuni na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, Juma Ali Khatibu, akizungumzia uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba 2024.

Khatibu alisema viongozi wa baraza hilo wanatekeleza falsafa ya R4 ya Rais Samia, inayojumusha maridhiano na kwamba wasimamizi hao wanapaswa pia wafundishwe namna ya kuzitekeleza.

“Sisi kama viongozi wa vyama vya siasa tunakwenda na R4 za Rais Samia na watendaji watakaokuwa na dhamana ya kusimamia uchaguzi na wao wapewe mafunzo ya hizo R4 tusimharibie rais kutokana na maono yake na muelekeo wake,” alisema Khatibu na kuongeza:

“Rais amefungua nchi kisiasa na kiuchumi, amekuza demokrasia na sisi viongozi wa kisiasa twende sambamba na ridhaa yake ya kuleta maridhiano ya kisiasa.”

About The Author