September 19, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Binti wa Shinawatra achaguliwa waziri mkuu mpya

 

BUNGE la Thailand limemchagua Paetongtarn Shinawatra, binti wa bilionea na kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Thaksin Shinawatra, kuwa waziri mkuu. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Akiwa na umri wa miaka 37, Shinawatra, atakuwa waziri mkuu mwenye umri mdogo zaidi nchi humo na mwanamke wa pili kuwahi kushikilia wadhifa huo baada ya shangazi yake Yingluck.

Wabunge wamemuidhinisha Paetongtarn wa chama cha Pheu Thai kuwa waziri mkuu kwa kupata kura 319 dhidi ya 145 waliopinga.

Kuchaguliwa kwake kunatokea siku mbili tu baada ya Waziri Mkuu wa zamani Srettha Thavisin kuondolewa na mahakama ya kikatiba.

Waziri Mkuu huyo mpya anakabiliwa na kibarua kigumu cha kufufua uchumi wa Thailand na kuepuka mapinduzi ya kijeshi na uingiliaji kati wa mahakama ambao umeondoa tawala nne zilizopita.

Thaksin Shinawatra alihudumu kama Waziri Mkuu wa Thailand kutoka 2001 hadi 2006. Baada ya kuondolewa madarakani, alipatikana na hatia ya ufisadi mwaka 2008 na sasa anaishi katika uhamishoni.

Dada yake mdogo Yingluck Shinawatra alikuwa waziri mkuu wa Thailand kutoka 2011 hadi 2014.

About The Author