STAA wa muziki wa AfroPop Yemi Alade ametoa albamu yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Rebel Queen’ ambayo inapatikana kupitia mtandao wa muziki wa Effyzzie Music. Anaripoti Joseph Shaluwa, Dar es Salaam … (endelea).
Katika albamu hiyo amewashirikisha nyota kadhaa wa muziki duniani, akiwemo gwiji Ziggy Marley ambaye ni mtoto wa mkali wa Regger wa muda wote, Bob Marley.
Jina la albamu hiyo ‘Rebel Queen’ ni ushuhuda wa utawala wa Yemi kama Malkia wa Afrika wa AfroPop, mwenye upendo wa dhati kwa bara la Afrika.
“Kuwa mpinzani ni kusafiri katika njia ngumu. Ni kuendelea kuwa mwaminifu kwako mwenyewe hata wakati wa kufanya chaguzi binafsi, bila kujali watu watasemaje,” anasema Yemi.
Wimbo “Peace & Love” aliomshirikisha mwanamuziki wa Jamaika, Ziggy Marley ambaye ni mshindi wa mara 8 wa Grammy, unazidisha ladha ya albamu hiyo.
Kibao cha kwanza kabisa kuachiliwa katika albamu hiyo, kiitwacho “Tomorrow” tayari kimeshaonesha mafanikio makubwa, kwani katika kipindi cha mwezi mmoja tangu kuachiwa hewani, tayari kimeshatazamwa na watu zaidi ya milioni 7.5.
Albamu hiyo yenye nyimbo 16 imewashirikisha mastaa wengine wakiwemo, Konshens & Femi One katika “Baddie Remix”, Angelique Kidjo katika “African Woman” na Innoss’B katika “Lipeka”.
Ni albamu yenye mchanyato mkubwa wa muziki, kuanzia AfroPop, Dancehall, Amapiano, Lingala, Afrobeats, Reggae na R&B, ambayo kwa hakika inakidhi haja ya msikilizaji kutokana na ladha za kila aina ya muziki ndani yake.
Yemi Alade anasema, “Nilitiwa moyo na muziki wa hadhi ya juu ya Kiafrika… nimetoa albamu hii kwa nia moja tu ya kutengeneza muziki ambao nilikuwa nikiupenda na aina ambayo ninaipenda mpaka sasa.”
Sikiliza kupitia hapa: https://idol-io.ffm.to/rebelqueen
ZINAZOFANANA
Liverpool yapewa nafasi kubwa ya ubingwa EPL
Jogoo Veterean yafurahia ujio wa Meridianbet
Wikendi inaanza kwa kubashiri na Meridianbet leo