December 11, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Thomas Mlugu aaga michuano ya Olimpics

Tegemeo la Watanzania kuchukua Medali kwenye Judo imefika mwisho baada ya Thomas Mlugu ambaye alitinga hatua ya 16 bora kwa kumpiga William Tin Tan na kuvuka hatua ya makundi kupoteza pambano mbele ya Mfaransa Gaba.

Licha ya Mlugu kuanza vyema kwa kuibuka na ushindi katika hatua ya 32 kwenye mchezo wa Judo, Mlugu amepoteza pambano lake la hatua ya 16 bora dhidi ya Joan-Benjamin Gaba na kuikosesha Tanzania medali ya kwanza kwenye michezo hiyo.

Mtanzania huyo alipita raundi ya 64 bora bila kucheza, kitu ambacho kilifanya Watanzania wengi kuwa na matumaini ya juu kwa mchezaji huyo kuipeperusha bendera ya Tanzania vizuri kupata medali baada ya mchezaji huyo wa judo kuibuka na ushindi wa pointi 10-1 dhidi ya William Tai Tin wa Samoa.

Michezo ya Olimpics 2024 inaendelea leo hii ambapo Taifa la Tanzania litamtazama Thomas Andrew Mlugu anayepeperusha vyema bendera ya Tanzania. Cheza pia michezo ya Kasino mtandaoni kama vile, Poker, Super Heli, Roulette, Aviator, Wild Icy Fruits, Keno na mingine kibao.

Mlugu alijikuta akipoteza pambano la raundi ya 16 bora dhidi ya Gaba wa Ufaransa kwa kuchapwa pointi 10-0 na hivyo kuaga mashindano hayo. Baada ya Mlugu kukosa pointi, matumaini ya Watanzania sasa yamehamia kwa wakimbiaji Gabriel Geay, Alphonce Simbu, Jackline Sakilu na Magdalena Shauri pamoja na waogeleaji Collins Saliboko na Sophia Latiff. Jisajili hapa.

Hapo kesho sasa, Saliboko ataiwakilisha Tanzania wakati atakapokata maji kwenye mita 100 free style na Ijumaa ijayo, Latiff atapeperusha bendera katika mita 50 free style. Hadi sasa, Marekani ndio inaongoza kwa kutwaa medali ikiwa nazo 12 ikifuatiwa na China iliyokusanya medali tisa.

Mwenyeji wa mashindano haya Ufaransa ina medali nane na Japan na Korea Kusini kila moja ina medali saba kibindoni.Bashiri sasa na Meridianbet.

Nchi ambazo zina medali sita kila moja ni Australia na Italia wakati Uingereza ikiwa na medali tano.

Pia Canada, Brazil na Kazakhstan kila moja ina medali tatu na Ubelgiji ina medali mbili huku nchi zenye medali mojamoja zikiwa ni Ujerumani, Hong Kong na Uzbekistan.

About The Author

error: Content is protected !!