RAIS mstaafu Jakaya Kikwete amesema amempongeza Rais Samia Suuhu Hassan kwa kubeba mzigo mzito katika kukamilisha mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma, huku vipande vingine vikiwa katika hatua mbalimbali za utekelezaji. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Kikwete ametoa kauli hiyo jana Jumatatu wakati akijibu swali la Idriss Sultan katika Podcast maalumu iliyofanyika nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.
Rais huyo wa awamu ya nne, amesema wazo la SGR lilianza baada ya Rais Mstaafu Benjamini Mkapa kufanya mazungumzo na Rais wa Rwanda, Paul Kagame juu ya kujenga reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam hadi Kigali.
Hata hivyo, Kikwete amesema “tumpongeze Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kubeba mzigo mzito katika kukamilisha mradi huo utakaogharimu takriban Dola za Marekani bilioni 7,” amesema.
ZINAZOFANANA
Ushindi wa Profesa Lipumba wapingwa
Sativa amlipia Lissu fomu ya kugombea Uenyekiti Chadema
John Tendwa afariki dunia