IDARA ya Marekani ambayo inamlinda Rais na Maafisa wengine wa sasa na wa zamani, wanachunguza ripoti ya milio ya risasi iliyosikika karibu na Ikulu ya White House.Anaripoti mwandishi wetu,Dar es Salaam …(endelea).
Maajenti wa Secret Service walijibu ripoti ya milio ya risasi katika eneo karibu na Lafayette Park huko Washington DC, muda mfupi baada ya saa sita usiku, na kupekua bustani hiyo, Kaskazini mwa Ikulu ya White House na eneo jirani.
Shirika hilo lilisema hakuna mshukiwa aliyepatikana na hakuna majeruhi walioripotiwa. Wakala na washirika wake wanawatafuta washukiwa.
Rais wa Marekani Donald Trump alikuwa Washington DC mwishoni mwa juma.
Shirika hilo la siri lilisema shughuli zake bado zinaendelea kama kawaida na hatua za usalama zimechukuliwa.
Anthony Guglielmi, Msemaji wa huduma ya siri, alisema kwenye mitandao ya kijamii kwamba awali baadhi ya barabara zilikuwa zimefungwa lakini kwasasa zimefunguliwa.
ZINAZOFANANA
Bei ya mafuta yashuka duniani
Vita yasitishwa, Iran yajiona mshindi
Trump atoa tishio jipya kwa Iran