Yoweri Museveni
“LISHE ya mihogo, viazi vitamu na mboga za asili zimenisaidia kupunguza kilo 30,” ameeleza Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, amenukuliwa na Idhaa ya Kiswahili ya BBC. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
“Afya yangu imekuwa nzuri kila wakati, lakini madaktari walifanya makosa na kisha nikaamua kupunguza uzito,” ameeleza Bw. Museveni.
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 75 awali hakuwa na ufahamu wa uzito wake, ambao ulikuwa ni kilo 106. Alisema, uzito wake wa sasa ni kilo 76, unaolingana na urefu wake wa futi 5 na inchi 7 (170cm).
Amekanusha maoni kwenye mitandao ya kijamii kwamba “anaonekana mchovu,” akisema amepunguza uzito kidogo tu.
Alisema kwenye blogu yake ya kibinafsi mwezi uliopita: “Nimekwepa kuwa na mwili mnene, kwa sababu madaktari hawakunielezea kuwa hii inasababisha matatizo au kwamba ni lazima kukabiliana na unene kupita kiasi.”
Hata hivyo, Rais Museveni hakueleza ni muda gani uliochukua kupunguza kilo 30.
“Ninakula mihogo kwa sababu sili chakula chenu cha Ulaya au Asia. Ninakula chakula chetu kama; mihogo, ndizi, viazi na mboga zetu za asili,” alisema Museveni.
ZINAZOFANANA
Netanyahu achezea kipigo, aomba msaada mataifa mengine
Iran yathibitisha kuwa Waziri wa Ujasusi ameuawa
Mojtaba Khamenei yuko salama kiafya na anaongoza kikamilifu – Iran