SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu nchini Senegal (FSF) limejitokeza kupinga kwa nguvu zote uamuzi wa Kamati ya Rufaa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) uliotolewa tarehe 17 Machi 2026, kufuatia shauri la fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2025 kati ya Senegal na Morocco. Anaripoti Joyce Ndeki, Dar es Salaam … (endelea).
Kwa mujibu wa CAF, uchunguzi wake ulibaini kuwa Senegal ilikiuka vifungu vya 82 na 84 vya kanuni za mashindano hayo, hali iliyosababisha timu hiyo kuadhibiwa kwa kupokonywa ushindi na kuipa Morocco ushindi wa mezani wa mabao 3-0.
Hata hivyo, FSF imekataa vikali uamuzi huo, ikiutaja kuwa hauna msingi wa haki, ni wa upendeleo na unaotia doa hadhi ya soka la Afrika mbele ya jumuiya ya kimataifa.
Katika hatua ya kusaka haki, FSF imetangaza kupeleka rufaa katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) yenye makao yake Lausanne, Uswisi, kwa matumaini ya kupata uamuzi wa mwisho wenye usawa.
Pamoja na msimamo huo mkali, FSF imesisitiza kuwa itaendelea kuheshimu misingi ya uadilifu, uwazi na haki katika mchezo wa soka, huku ikiiahidi jamii ya wanamichezo barani Afrika kuendelea kutoa taarifa kadri mchakato wa kesi hiyo nyeti utakavyoendelea.
ZINAZOFANANA
Nani kwenda Robo Fainali UEFA leo?
Ndani ya Meridianbet leo utaweza kuibuka na ushindi ukiwa nyumbani
Man Utd, Liverpool kuwezesha bahati yako ndani ya Meridianbet leo