February 2, 2026

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Watu 100 wameuawawa shambulio la kukamatwa Maduro

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Venezuela, Diosdado Cabello

 

WAZIRI wa Mambo ya Ndani wa Venezuela, Diosdado Cabello amesema, takribani watu 100 wameuawawa katika shambulio la Marekani la Jumamosi lililomuondoa madarakani, Rais Nicolás Maduro. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Serikali ya taifa hilo haikuwa imetoa idadi ya waliouawa hapo awali, lakini jeshi lilichapisha orodha ya majina 23 ya wanajeshi wake waliokufa.

Maafisa wa Venezuela wamesema sehemu kubwa ya kikosi cha ulinzi cha Maduro kiliuawa “kikatili,” na Cuba imesema wanajeshi na maafisa wake wa kijasusi 32 waliokuwa Venezuela waliuawa.

Mke wa Maduro, Cilia Flores, aliyekamatwa pamoja naye, alipata jeraha la kichwa wakati wa uvamizi wa Marekani na Maduro alipata jeraha kwenye mguu wake.

Jumanne iliyopita Rais wa mpito wa Venezuela, Delcy Rodriguez alitangaza wiki moja ya maombolezo kwa wanajeshi waliouawa katika uvamizi huo.

About The Author

error: Content is protected !!