December 2, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Simba yaachana na Pantev, aiongoza kwa mechi tano

Dimitar Pandev

UONGOZI wa Klabu ya Simba umechana na Meneja wake Mkuu, Dimitar Pantev na wasaidizi wake wawili, baada ya kuiongoza timu hiyo kwa mechi tano pekee. Anaripoti Fedrick Gama, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa iliyotolewa na Bosi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo, leo tarehe 2 Desemba, 2025, kutokana na matokeo mabovu waliyopata timu hiyo, ikiwa pamoja na kupoteza michezo miwili ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Pantev alitambulishwa rasmi tarehe 3 Oktoba 2025, akichukua mikoba ya Fadlu Davids, kufuatia mabadiliko ya kiutendaji katika benchi la ufundi la klabu hiyo.

Safari yake katika klabu ya Simba imedumu kwa takriban miezi miwili kamili tangu alipowasili Dar es Salaam.

Pandev alianza kuiongoza Simba katika mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika Nsingizini Hotspurs Eswatini na kushinda mabao 3-0 kabla ya kurudiana jijini Dar es Salaam na kumaliza kwa suluhu.

Baada ya michuano ya Kimataifa, Pantev alikuwa katika benchi la Simba dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Pantev aliiongoza pia Simba katika michezo miwili ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kupoteza dhidi ya Petro de Luanda ya Angola na Stade Malien ya Mali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bodi ya Wakurugenzi ya klabu ya Simba, kikosi hicho kitakuwa chini ya Seleman Matola mpaka atakapopatikana kocha mwingine.

About The Author

error: Content is protected !!