
SERIKALI ya Tanzania imekamilisha ukarabati wa uwanja wa mpira wa miguu wa Benjamin Mkapa. Anaripoti Fredrick Gama, Dar es Salaam … (endelea).
Ukarabati huo, umegharimu takribani Sh. 31 bilioni na kwamba mradi huo mkubwa umelenga kuifanya Tanzania kuwa mwenyeji bora wa mashindano ya CHAN 2025 na AFCON 2027.
Taarifa ya serikali imesema, mradi huo umekamilika kwa awamu mbili tofauti, ambapo awali ilitengwa Sh. 7.44 bilioni na baadaye kutumika kiasi kingine kilichosalia.
“Lengo kuu la Serikali lilikuwa ni kuhakikisha miundombinu ya michezo inakidhi vigezo vya kimataifa na kuchangia katika ukuaji wa kiuchumi,” imeeleza taarifa hiyo ya serikali.
Ukarabati huu sio tu umeboresha miundombinu ya michezo nchini, bali pia umetoa ajira za muda kwa wananchi 1,200. Ajira hizo zilijumuisha mafundi, wahandisi na wasimamizi wa ujenzi.
Audha, ajira 150 za kudumu zimetolewa kwa ajili ya usimamizi na matengenezo ya uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 60,000.
Uwanja wa Mkapa unatarajiwa kuchangia kukuza uchumi wa ndani kupitia sekta ya utalii na biashara.
ZINAZOFANANA
Jiji la Dodoma kupata uwanja mpya wa kisasa wa michezo
Wananchi kuanza utetezi wa ubingwa NBCL leo
Europa League kukupeleka moja kwa moja kwenye ushindi wa Meridianbet.