
RAIS wa klabu ya Yanga Hersi Ally Said amesema kuwa, klabu hiyo ilikataa ofa ya kiasi cha Shilingi Bilioni 5 sawa na Dola elfu mbili, kwa ajili ya kumuuza mshambuliaji wa Clement Mzize. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).
Hersi amaeyasema hayo wakati akihutubia Mkutano mkuu wa klabu hiyo unaondelea hivi Sasa kwenye ukumbi wa Super Dom, Masaki Jijini Dar es Salaam.
Katika hotuba yake kwa wajumbe wa mkutano mkuu Hersi alisema kuwa, malengo ya Yanga kwa msimu huu ni makubwa hivyo wanamuhitaji mshambuliaji huyo licha ya uwepo wa ofa nyingi.
“Naomba niwaambie Wananchi Yanga sio ‘academy’ ya kuuza wachezji, sisi tunataka kupata mafanikio, tunamuhitaji sana Mzize msimu huu,” alisema.
Aidha Hesri alisisitiza kuwa mchezaji huyo kwa Sasa hauzwi kwa bei yoyote labda mwisho mwa msimu huu wa 2025/26 watafikilia kufanya biashara.
“Ofa ya mwisho ya Mzize ilikuja ya dola Milioni 2, lakini tukasema hauzwi kwa bei yoyote, tunahitaji mafanikio hatuwezi kuuza silaha zetu, msimu huu ukiisha tunaweza kufikilia kufanya biashara.” alisema Hersi.
Mchezaji huyo kwa sasa yupo kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania, ambacho kinasaka tiketi ya kufuzu fainali za kombe la Dunia.
ZINAZOFANANA
Mechi za kufuzu Kombe la Dunia kukupatia ushindi
Walii aingiza filamu ya ‘Mke wa Mama’ mtaani
Thamani ya klabu ya Yanga yafikia Sh. 100 Bilioni