
MABINGWA wa zamani wa dunia katika Masumbwi, Mike Tyson na Floyd Mayweather wanatarajiwa kurudi ulingoni kwa pambano la ridhaa la maonyesho mwaka 2026. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Tyson aliwahi kuwa Bingwa wa uzito wa juu dunaini, anarudi baada ya kumbukumbu ya kupoteza kwa pointi dhidi ya Jake Paul katika pambano la raundi nane lililofanyika Novemba 2024.
Kwa upande wake, Mayweather alitawala aina tano za viwango vya uzito na kustaafu bila kupoteza pambano, akivunja rekodi ya mapambano 50 bila kushindwa, alimaliza rasmi safari yake ya ulingoni mwaka 2017 baada ya kumshinda Bondia wa MMA, Conor McGregor.
Hata hivyo, licha ya heshima ya historia zao kubwa, Tyson na Mayweather hawajawahi kukutana ulingoni katika kipindi cha ushindani wao kutokana na tofauti ya viwango vya uzito na vipindi vyao vya kushiriki mchezo.
Pambano hili la maonyesho la mwaka 2026 linatarajiwa kuvutia hisia kubwa kutoka kwa mashabiki duniani kote,likiwa ni tukio la kipekee la kuwakutanisha mabondia wawili maarufu zaidi katika historia ya mchezo wa masumbwi.
ZINAZOFANANA
Mechi za kufuzu WC Ulaya kukupatia mkwanja leo
Magori mwenyekiti mpya Bodi ya Simba, Barbara ndani
Rais mstaafu Peru ahukumiwa miaka 13 jela