
Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kesho kinatarajia kufanya harambee ya kukusanya fedha zitakazosaidia kampeni za uchaguzi mkuu utakaofanyika mwishoni mwa mwaka huu. Anaripoti Salehe Mohammed, Dar es Salaam … (endelea).
Mpango huo umebainishwa leo, jijini Dar es Salaam na Katibu wa CCM, Dk Emmanuel Nchimbi alipokuwa akizungumza na wahariri na waandishi wa habari ambapo amesema lengo hilo ni kuhakikisha kila mwanachama anashiriki kwenye maendeleo ya chama.
“Sisi tunataka kuonyesha mfano wa chama imara kinachowashirikisha wanachama katika maendeleo ya chama chao” amesema
Amesema chama hivi sasa kinafanya maandalizi ya kampeni hivyo wanahitaji fedha na rasilimali watu.
“Tunatarajia kampeni zichangamke sana, tumepata michango kutoka kwa wanachama ambayo tutaitumia katika kununua tisheti, kofia, kanga fulana na vifaa vinginevyo” anasema.
Dk Nchimbi amesema kuwa mpaka leo wanachama waliosajiliwa kidijitali ni 13.19 hivyo katika harambee hiyo wanatarajia kupata fedha nyingi zaidi.
Wanaifanya kesho ukumbi wa Mlimani City ambapo Rais Samia ni mgeni rasmi kwa kuwa wanajua wenye uchungu na chama chao
“Kesho ndiyo siku ya wanachama kuonyesha nguvu yao ili kufikia maendeleo ya nchi na chama chao”
Amesema kuna hamasa kubwa miongoni mwa wanachama na wanajivunia tukio hilo.
Amesema kuwa CCM watadhibiti fedha za wageni ambazo hazina lengo zuri.
“Tutaanisha michango ya wageni ile inayodhalilisha na kushusha heshima ya Watanzania tutaachana nayo”
“Sisi hatupigi minada zetu ili kupata fedha za kugharimia kampeni. Watu wote tunawapata nafasi ya kuchangia” amesema.
Amesema kuwa watakaochangia kidogo na kikubwa wote wataheshimiwa na kupokea michango yao kwa ajili ya harambee.
“Heshima ya chama chetu huwezi kuiuza ni kubwa, hatuwezi kuiuza. Watu wenye mapenzi na sisi tunawakaribisha watuchangie” amesema.
ZINAZOFANANA
EXIM yatangaza mafanikio makubwa na mwelekeo madhubuti 2025
Cheza Expanse kasino na utajirike
Sloti ya Veni Vidi Vici inatajirisha kirahisi