December 18, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Moto wa Chelsea waendelea kuwaka huko Uingereza

Chelsea FC kutoka pale Uingereza imeendelea kufanya maajabu ambayo watu wengi hawakutarajia kutokana na misimu miwili mibovu nyuma ambayo walipitia toka alipoondoka Thomas Tuchel.

The Blues msimu wa 2021 waliweza kupata mafanikio makubwa chini ya kocha wa Kijerumani Tuchel ambaye msimu wake wa kwanza aliweza kubeba mataji makubwa ya UEFA SUPER CUP pamoja na FIFA CLUB WORD CUP. Lakini hata hivyo kocha huyo hakudumu klabuni hapo na hatimaye 2022 Septemba Graham Potter alichaguliwa kuwa kocha mkuu wa vijana wa Darajani kutoka Brighton.

Baada ya Potter kutua Chelsea aliweza kuungana na mchezaji wake Marc Cucurela ambaye kwasasa ni moja ya wachezaji tegemezi wa klabu hiyo. Lakini pia klabu hiyo iliweza kuwasajili wachezaji wengi akiwemo Koulibaly, Wesley Fofana, Sterling na wengine kibao lakini pia kocha huyo alishindwa kuifikisha timu hiyo top 6.

Ili kupiga pesa nyingi, endelea kubashiri na Meridianbet ambapo ODDS KUBWA na machaguo zaidi ya 1000 yapo hapa. Pia cheza michezo ya Kasino ya mtandaoni kama vile, Poker, Super Heli, Roullette, Aviator, Wild Icy Fruits, Keno na mingine kibao.

Muwekezaji mpya wa Chelsea Toddy Boehly aliamua kumleta Mauricio Pochettino kwaajili ya kuinoa Chelsea ambapo ndani ya msimu mpya wa 2023 klabu hiyo ilirudi sokoni na kufanya usajili mkubwa kabisa ikiwa ni timu pekee ambayo imetumia pesa nyingi zaidi kufanya usajili.

Baadhi ya wachezaji ambao walisajiliwa msimu huo ni pamoja na Enzo Fernandez, Mudryk, Malo Gusto, Noni Madueke, Cole Palmer ambaye alichukua tuzo ya mchezaji bora chipukizi, Joao Felix kwa mkopo na wengine kibao ambao akiwemo Nkunku ambao walikuja kuisaidia timu hiyo.

Pochettino alijitahidi sana kuiweka Chelsea kwenye nafasi nzuri ambapo walishindwa kufuzu kucheza ligi ya mabingwa na hatimaye kuangukia kucheza EUROPA CONFERENCE LEAGUE.

Hatimaye The Blues baada ya msimu kuisha waliamua kuachana na Pochettino na kumsajili Enzo Maresca ambaye aliipandisha daraja Leicester ambapo walikuwa na matumaini ya kufanya vizuri.

Enzo Maresca alianza kwa kichapo kabisa mechi yake ya kwanza dhidi ya bingwa mtetezi Manchester City, huku mechi yake ya pili akitoa sare.

The Blues kutoka pale Stamford Bridge wakiwa wamewekeza kwenye vijana wadogo hatimaye mwanga ulianza kuonekana kwao na kuanza kushinda mechi zao ambapo mpaka sasa wapo nafasi ya 2 kwenye msimamo wa ligi, wakishinda mechi 10, sare 4 na kupoteza 2 kwenye michezo 16.

Pia ndiyo timu ambayo imefunga magoli mengi kuliko yoyote EPL wakifunga magoli 37, wakati mchezaji wao wa Kiingereza Cole Palmer akiweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Uingereza kufunga magoli manne kipindi cha kwanza cha mchezo ambapo alifanya hivyo mechi dhidi ya Brighton.

Kule kwenye CONFERENCE LEAGUE wameshinda mechi zote 5 na kukusanya pointi zao 15 na kuwa kileleni pale kwenye msimamo.

Lakini kwenye mahojiano ambayo kocha mkuu Enzo anafanya bado anakiri kuwa timu yake bado haiko kwenye mbio za ubingwa ila inachotaka ni kukusanya pointi 3 pekee. Je Chelsea msimu huu itamaliza nafasi ya ngapi?. Je itaweza kubeba ligi mbele ya Liverpool ambao ndio vinara wa ligi hadi sasa?

About The Author

error: Content is protected !!