SERIKALI ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na vyombo vya habari vya taifa hilo vinasema, makubaliano ya kusitisha mashambulizi kwa muda ni ushindi mkubwa kwa wananchi wake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Katika taarifa iliyotolewa na Baraza Kuu la Usalama wa Taifa, Iran imesema imeafikia karibu malengo yake yote ya vita hivyo na kwamba adui wake amepata pigo la kihistoria.
“Tumeshinda. Tumeshinda. Tumeweza kustahimili vita vilivyoanzishwa na Israel na Marekani kwa zaidi ya siku 30. Haya siyo mafanikio madogo,” ameeleza kiongozi mmoja wa kijeshi ambaye hakupenda kutajwa jina lake.
Vita dhidi ya Iran vilianza tarehe 28 Februari kwa kuuawa Kiongozi Mkuu wa taifa hilo, Ali Khamenei, pamoja na viongozi wengine wakuu wakijeshi, vilikuwa tishio kubwa kwa utawala wa Iran.
Wakati Iran ijivunia ushindi wake, Rais Donald Trump wa Marekani, naye amesema hakuna shaka kwamba Marekani imepata “ushindi kamili” baada ya kukubaliana kuhusu kusitisha vita kwa wiki mbili.
Katika mahojiano na Agence France Presse baada ya tangazo lake, alisema kwamba urani iliyorutubishwa ya Iran “itajadiliwa kikamilifu” chini ya makubaliano hayo.
“Vinginevyo nisingekubali,” alisema Trump bila kutoa maelezo yoyote kuhusu kile ambacho kingetokea kwa Iran.
Alipoulizwa kama angerudi kutoa tena vitisho kama vya awali vya kuharibu mitambo ya nishati na madaraja ya Iran ikiwa makubaliano yangevunjika, aliishia kusema, “Utalazimika kufuatilia hili.”
Trump, ambaye anatarajiwa kusafiri hadi China mwezi ujao kukutana na mwenzake Xi Jinping, alisema: “Nasikia hivyo.”
Alikuwa akijibu swali kuhusu ushiriki wa Beijing katika kumfanya mshirika wake mkuu Tehran kujadiliana juu ya makubaliano ya usitishaji wa mapigano.
ZINAZOFANANA
Trump atoa tishio jipya kwa Iran
Rais wa Sudan kusin,amtimua Spika na Naibu Spika
Gavana wa zamani Urusi ahukumiwa miaka 14 Gerezani kwa Rushwa