February 23, 2026

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Rais Kiir ateuwa aliyekufa miaka 5 iliyopita kusimamia uchaguzi

 

RAIS wa Sudan Kusini, Salva Kiir amemteua mtu aliyekufa kuwa mjumbe wa kamati itakayoandaa uchaguzi wa nchi yake. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Msemaji wa ofisi ya rais, amesema kwamba Rais Kiir amemteua bila kukusudia mtu aliyekufa kuwa mjumbe wa kamati itakayoandaa uchaguzi wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Amesema, mamlaka zilipitiwa wakati wa uteuzi baada ya Steward Sorobia Budia, mwanasiasa wa zamani wa upinzani kuwa miongoni mwa wajumbe waliotajwa katika amri iliyotolewa na Rais Kiir.

Budia alifariki miaka mitano iliyopita.

Taarifa zinasema familia ya marehemu sasa inadai fidia, kwa kuzingatia tamaduni zinazokataza kuomba au ‘kuamsha’ roho ya marehemu bila ufahamu, ridhaa au ushiriki wa familia.

Hakujawahi kufanyika uchaguzi nchini Sudan Kusini iliyopata uhuru tangu 2011, katika nchi  ambayo imekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vya kila mara.

About The Author

error: Content is protected !!